title : QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018
kiungo : QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018
QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018
Kinyang'anyiro cha kumpata mrembo wa Miss Tanzania 2018 limefanyika jana usiku na Mrembo kutoka Kinondoni Queen Elizabeth amefanikiwa kuondoka na taji hilo katika shindano lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Saalaam.
Katika shindano hili, Mshindi wa pili ni Nelly Kazikazi na mshindi wa tatu ni Sandra Giovinazzo., nafasi ya nne ikienda kwa Teddy Nkenda na wa tano ni
Baada ya kuibuka na ushind wa taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth ameweka wazi mwanzo mwisho kile kilichopelekea kushinda taji hili la U-Miss kwa walikuwa wanashindana na warembo wengi halafu wazuri.
“Nafurahia kushinda taji hili la Miss Tanzania 2018, najisikia vizuri sana napenda kuwashukuru majaji kwa kuweza kuona nafaa kuiwakilisha nchi nasema asante Tanzania, ukiwa kama mrembo lazima ujiandae kama unavyoona warembo ni wazuri sio kwamba ni wazuri kumuonekano tu hata kichwani pia wako vizuri” Queen alisema
Katika shinda no hilo Queen Elizabeth amewashinda warembo wengine 19 waliokuwa wakiliwinda taji hilo kubwa kabisa nchini katika tasnia ya urembo.
Shindano la Miss Tanzania 2018 liliweza kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiwa moja ya zao la Miss Tanzania 2006 na kuibuka namba mbili Jokate Mwegelo pamoja mbunge wa Segerea Bona Kaluwa.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa, mashindano ya mwaka huu yamekuwa na tija kubwa sana kutokana na waandaaji wa mwaka huu chini ya Basila Mwanukuzi kujipanga na kushirikiana na serikali kuanzia hatua ya mwanzo mpaka kufikia tamati.
Warembo watano waliofanikiwa kuingia tano bora wamepewa ubalozi wa mwaka mmoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Misitu Nchini (TFS).
BOFYA HAPA KUONA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA ZAIDI
Hivyo makala QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018
yaani makala yote QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/queen-elizabeth-ashinda-taji-la-miss.html
0 Response to "QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018"
Post a Comment