WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016
kiungo : WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016

soma pia


WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016


Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

CPA. Mwakapalila alisema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa hizo katika kufanya maamuzi.‘Kama taarifa za fedha hazitatolewa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati mwafaka kunaweza kusababisha athari katika uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini’, alieleza CPA. Mwakapalila

Aidha Mwakapalila amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

Amesema suala la Uchumi wa viwanda ni muhimu katika kuongeza kipato na kupata fedha za kigeni kwa njia ya kuuza bidhaa nje na pia kupata mapato ya kodi na yasiyo ya kodi hivyo akatoa rai kwa wananchi kuendelea kujadili masuala ya uchumi wa viwanda na kupata namna sahihi ya kuufikia ili ndoto ya uchumi huo ziweze kuwa za kweli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno amesema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa.

Amesema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.
Wahasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 wakiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto) baada ya kupokea Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zilizotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam .
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahasibu wa Wizara hiyo fungu 50 baada ya kuwakabidhi tuzo hiyo katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliyeshika tuzo ni Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama.
Washindi wa Kwanza wa makundi mbalimbali ya Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa wahasibu walioambatana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50, Bw. Christopher Nkupama (hayupo pichani) akisalimiana na meza kuu baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.



Hivyo makala WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016

yaani makala yote WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/wizara-ya-fedha-na-mipango-yaibuka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016"

Post a Comment