MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA

MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA
kiungo : MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA

soma pia


MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA

Na Karama Kenyunko,  blogu ya jamii

MWALIMU Mkuu wa  Shule  ya  Msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam na walimu  wake wanne wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu.

Sababu za kupandishwa kizimbani inatokana na kutakiwa  kujibu  tuhuma za kupata  mitihani ya Taifa ya darasa la saba na kufanya mawasiliano ya maudhui yake na watahiniwa wa shule hiyo isivyo halali.

Mwalimu Mkuu huyo Patrick Cheche (43) Wa shule hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikitangazwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya darasa la nne na la saba na walimu wenzake wamesomewa mashtaka yao leo mbele  ya  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi Huruma  Shahidi.

Mbali na Cheche (43), anayeishi Mpinga Bagamoyo, washtakiwa wengine ni Laurence Ochien (30), Justus James (32), Nasri Mohamed (32) na Mambo Idd (32), ambao wote wakazi wa Dar es Salaam.

Akisoma hati  ya  mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi  Mutalemwa Kishenyi  akisaidiana na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai washitakiwa hao Septemba 4, mwaka huu, katika Jiji na Mkoa wa  Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama  ya kutenda kosa la kuingilia mitihani ya Taifa ya darasa la saba isivyo halali.

Washtakiwa katika Shtaka hilo la  kula njama wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kanuni za adhabu.

Katika shtaka la pili ambao washtakiwa hao wanashitakiwa chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa, wanadaiwa Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo ya Hazina, iliyoko Magomeni, kujibu, kinyume cha sheria walipata uwezo wa kupata mitihani wa taifa wa darasa la saba na kuonesha maudhui yake kwa watahiniwa waliosajiliwa Katina shule hiyo.

Pia imedaiwa Katika shtaka la tatu, Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo washtakiwa hao kwa makusudi walitoa mitihani kwa watahiniwa waliosajiliwa katika shule hiyo wakati hawakustahili kufanya hivyo.Hata hivyo washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo  na wako  nje kwa dhamana.

 Kwa Mujibu wa  upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Akisoma masharti ya dhamana,  Hakimu Shaidi amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana, kila mmoja anatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho, vitambulisho na mmoja kati ya wadhamini hao awe anatambulika katika taasisi yoyote.

Pia kila mdhamini anatakiwa kusaini bondi ya Sh.milioni sita na mshtakiwa wa kwanza na wa pili watatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria kwani wao ni raia wa Kenya.Hata hivyo washtakiwa hao walifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana kasoro mshtakiwa wa pili  ambaye alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama laa.

 Mwalimu Mkuu wa  Shule  ya  Msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam na walimu  wake wanne wakipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu mapema leo.


Hivyo makala MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA

yaani makala yote MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mwalimu-mkuu-shule-ya-msingi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI YA KIMATAIFA HAZINA ,WALIMU WANNE KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUPATA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA"

Post a Comment