title : RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO
kiungo : RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO
RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO
*Fly Over ya kwanza kujengwa nchini ,wananchi Dar watoa ya moyoni kwa Rais
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
FLY Over ya kwanza kujengwa nchini Tanzania inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Rais Dk.John Magufuli.
Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni wazi Tanzania imeingia kwenye historia ya aina yake katika kuhakikisha inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza adha ya msongamano wa magari.
Kwa sasa wananchi wa Dar es Salaam ambao wanapita katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere tayari wameanza kuonya raha ya uwepo wa Fly over hiyo iliyopo Tazara na kesho ndio siku ya uzinduzi rasmi.
Taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari jana na leo inaelezwa kuwa uzinduzi huo wa Fly Over ya Tazara utafanyika kesho asubuhi.Fly Over hiyo tayari imepewa jina la Mfugale.
Wakati uzinduzi huo ukisubiriwa kwa hamu na Watanzania na hasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu kukamilika kwa Fly over hiyo.
Wakizungumza zaidi na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wananchi wamesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa Fly Over hiyo unakamilika kwa wakati.
Wamesema wameanza kuona namna ambavyo kero ya msongamano wa magari iliyokuwepo eneo la Tazara ambayo kwa sasa haipo tena.
"Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo Serikali yake ilivyodhamiria kuboresha maisha ya wananchi na hasa katika hili la ujenzi wa miundombinu.Imesaidia kutuondolea adha ya kutumia muda mwingi katika foleni ya Tazara ambayo kwetu ilikuwa kero kubwa.
" Nchi yetu imeingia kwenye historia ambapo sasa nasi Watanzania tunayo nafasi ya kujivunia kukamilika kwa Fly Over hii ya Tazara,"amesema Shaban Chuma mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Jamila Jonathan amesema hakuwa akifikiria kama ipo siku katika Jiji la Dar es Salaam kutakuwa na Fly over lakini anamshukuru Rais kwani ameweza kufanikisha hilo.
"Nimesikia kesho ndio inazinduliwa rasmi.Nashukuru binafsi nimeonja raha ya kupita katika Fly over ya Tazara.Hongera Rais wetu kwa kutuondolea foleni iliyokuwa Tazara," amesema Jonathan ambaye ni Mkazi wa Pugu Stesheni.
Ameongeza anatamani kuona katika makutano yote ambayo yanachangamoto kubwa ya msongamano basi yanakuwa na Fly over huku akieleza anafahamu kuwa kuna ujenzi unaendelea Ubungo ambao lengo ni kupu guza msongamano, hivyo anatoa pongezi kwa Serikali ya Rais Magufuli ambayo ikisema inatekeleza.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO
yaani makala yote RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/rais-magufuli-kufungua-rasmi-fly-over.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO"
Post a Comment