Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo
kiungo : Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo

soma pia


Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowasili Nchini leo Septemba 26, 2018 kwa ziara maalu. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na kushoto Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke.
NA ANDREW CHALE, DAR

MJUKUU wa Malkia wa Uingereza, Prnce William ametua Nchini Tanzania jioni ya leo Septemba 26, 2018 kwa ziara maalum ya siku tatu ambapo kesho Septemba 27, anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Prince William katika kukutana na Rais Magufuli atafanya mashauriano kuhusu juhudi zinazochukuliwa na Tanzania katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori.

Prince William ametua mchana wa leo na ujumbe wake ambapo amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Katiba Sheria Profes Kabudi  pamoja na viongozi wengine akiwemo Balozi wa Uingereza hapa Nchini na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha Nchi zao Nchini.

Akiwa uwanjani hapo wa Mwalimu Julius Nyerere eneo la wageni mashuhuri, Prince William amepata wasaha wa kuteta na viongozi hao kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mwanamfalme huyo, kesho hiyohiyo ya Septemba 27, anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es salaam katika kitengo cha Polisi Marine (Marine Polisi Unit) na ambapo pia atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo yale ya kupokelea mizigo, upekuzi na ukaguzi wa vinavyoingia na kutoka katika eneo hilo la bandari.

Pia Prince William anatarajiwa kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo Mpingo Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Prince William na ugeni wake huo unatarajiwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na baadae Chuo cha Wanyamapori cha Mwika (College of African Wildlife Management, Mwika (CAWM), kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na kisha kuendelea na ziara yake Nchini Kenya.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa lengo kuu ya ziara hiyo ya Prince William ni pamoja na kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama.

Prince William atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William akisalimiana na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki waliomwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Augustino Maige. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.


Hivyo makala Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo

yaani makala yote Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mjukuu-wa-malkia-wa-uingereza-prince.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo"

Post a Comment