title : MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU
kiungo : MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU
MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza n.a. wanafunzi wenye ulemavu wakati wa mahafli ya 45 ya shule ya msingi Wokovu iliyopo jijini hapa jana.
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameishauri serikali na Jamii kwa ujumla,Kuongeza jitihada za kuhakikisha kwamba watoto wenye ulemavu wanapata nafasi za kusoma na kutambulika sehemu mbalimbali.
Meya Mwita ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki Wakati wa mahafali ya 45 ya darasa lasaba katika shule ya walemavu ya Jeshi la Wokovu iliyopo jijini hapa ambapo alisema kuwa watu wenye ulemavu wanaonekana hawafai,hawapati nafasi katika jamii na hivyo kushauri jitihada mahususi zitumike kuwatambua watu hao.
Aliongeza kuwa katika sekta ya elimu ,Taasisi mbalimbali pamoja na mashirikia ya dini ndio zimekuwa mstari wa mbele kutoa nafasi za kupatiwa elimu kwa makundi hayo na kutoa wito kwa jamii nyingine kujitoa kusaidia makundi hayo.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimkabizi zawadi mwanafunzi mwenye ulemavu wa miguu Ernest aliyemaliza darasa la Saba jana katika shule ya msingi Wokovu.
" Kazi mnayoifanya nyie jeshi la Wokovu ilitakiwa ifanywe na Serikali,lakini kwa nafasi yenu mmeweza ndio mana leo hii tuko hapa,mnapaswa kupongezwa ,nitumie nafasi hii kuwaawlika viongozi wa serikali, mashirika mbalimbali kujitoa ili kusaidia shule hii ambayo imeonyesha nia dhabiti ya kusaidia watoto hawa" alisema Meya Mwita.
Aidha katika hatua nyingine Meya Mwita aliwataka wazazi waliokuwa na watoto wao shuleni hapo kuwa mabalozi kwa wazazi wengine na hivyo kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu kama wengine.
"Niwapongeze wazazi wenye watoto wenu hapa,
mmeonyesha uthubutu mkubwa,hizi sio dhama za kuficha watoto,waambieni na wengine wasiwafiche waleteni wapate elimu ili iwasaidie huko badae, hawa ndio watakuja kuwa viongozi wa badae"alisema Meya Mwita.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ,Mkurugenzi wa shule hiyo ,Luteni Thomas Sinana mbali na kumpongeza Meya Mwita kuhudhuria mahafali hayo,alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 210 wenye ulemavu huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali.
Alieleza changamoto hizo kuwa ni upungufu wa vitabu ,huku wanafunzi wengine wakishindwa kufika shuleni wakati wa likizo kutokana na kukosa Fedha za kuwasafirisha. Alifafanua kuwa shule hiyo inachukua wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo wakati mwingine huwawia vigumu wanafunzi hao kurudi shuleni kutokana na ukosefu wa Fedha hivyo kuiomba serikali kusaidia.
"Ndugu mgeni rasmini ,shule hii inachangamoto nyingi ,tunaomba utufikishie salam zetu kwa viongozi husika, awali serikali iliweka utaratibu wa kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kupatiwa fedha za kujikimu,lakini kwa sasa imeondoa,tunaomba utufikishie salam zetu huko" alisema Luteni Sinana.
Hivyo makala MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU
yaani makala yote MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/meya-mwita-aishauri-serikali-jamii.html
0 Response to "MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU"
Post a Comment