title : KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE
kiungo : KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE
KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akiwa katika uzinduzi wa albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma. Wageni wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda (kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) na Mbunge wa Tabora Mjini, Mhe. Emmanuel Mwakasaka.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda akizungumza na viongozi mbali mbali wa kitaifa, wanakwaya wa kwaya ya Upendo Sikonge ya Mkoani Tabora na waumini wa kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini ya Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akipokea risala aliyopatiwa na wana kwaya ya upendo kutoka kanisa la Moravain Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Tabora Mjini, Mhe. Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Mhe. Richard Mbogo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula. Katika Shughuli hiyo Katibu wa Bunge alimuwakilisha Spika Ndugai.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na wanakwaya na waumini wa kanisa la Moravian Iringa Road wakati wa uzinduzi wa Albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora iliyofanyika leo Jijini Dodoma. Katika Shughuli hiyo Katibu wa Bunge alimuwakilisha Spika Ndugai.
Hivyo makala KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE
yaani makala yote KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/katibu-kagaigai-mgeni-rasmi.html
0 Response to "KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE"
Post a Comment