title : Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake
kiungo : Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake
Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam
Paul Makonda, leo amesaini mikataba ya lishe na Wakuu wa Wilaya zake tano.
Akisaini mikataba hiyo Dar es Salaam Makonda alitoa wito kwa Wakuu wa Wilaya zote kuakikisha Manispaa zao zinafanya vizuri katika kuzingatia suala la lishe wanapoingia katika vikao vyao vya Baraza la Madiwani liwe sehemu ya ajenda kila siku.
"Leo katika Mkoa wangu tumesainiana mkataba na wakuu wa wilaya zangu wote na katika wilaya tano Temeke,Iĺala na Kinondoni ina idadi kubwa ya watoto ni changamoto elimu hii mtakayopata mkashushe katika jamii"alisema Makonda
Alizitaka Kamati za Afya wilaya zote kuzingatia usafi pamoja na Makatibu Tawala na wakuu wa wilaya sambamba na wakazi wake wa Mkoa Dar es salaam .
Aidha amewataka wanawake wajawazito kuzingatia lishe katika siku 1000 za ujauzito na miaka miwili ya ukuaji mtoto.
Kwa upande wake Ofisa Lishe Mkoa wa Dar es Salaam,Janeth Mzava alisema mkoa wa Dar es salaam una mikakati saba wa kutoa elimu ya lishe ngazi ya jamii pamoja na utoaji wa elimu huo pia kuongeza virutubisho katika vyakula.
Mzava alisema pia mkakati mwingine kuongeza matibabu katika Utapia mlo.
Alisema vyanzo vya fedha katika utekelezaji wa shuguli za lishe zinatokana na wadau na serikali,kupitia mapato ya ndani(OS)mapato ya matumizi mengine
(OC)na mfuko wa pamoja wa afya (HSBF)kupitia vyanzo vya serikali.
Alitaja Halmashauri iliyofanya vizuri katika mikakati ya lishe wilaya Temeke ya kwanza kwa kutoa fedha zilizotengwa,wilaya ya Ilala ya pili inaonyesha kutumia shilingi milioni 100 ĺakini wanaonekana wametumia milioni 44,Kigamboni milioni 27 lakini wametumia 2,460,000.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Grace Magembe alisema mara baada mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kusaini mkataba na wakuu wa wilaya ,kazi itakayobaki Wakuu wa wilaya wote kwenda kusaini mkataba wa lishe kwa Mkurugenzi wa manispaa pamoja na Mchumi awepo.
Hivyo makala Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake
yaani makala yote Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/makonda-asaini-mikataba-ya-lishe-na.html
0 Response to "Makonda asaini Mikataba ya lishe na Wakuu wa wilaya zake"
Post a Comment