title : Mafundi washauriwa kuwa waaminifu
kiungo : Mafundi washauriwa kuwa waaminifu
Mafundi washauriwa kuwa waaminifu
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Edson Fungo kwenye tai nyekundu akioneshwa jinsi injini ya gani inavyofanya kazi na mwanafunzi aliyehitimu Mussa Ally.
Na Mwandishi WETU
WANACHUO wa Bruno Vocational Training Centre (BVTC) wameshauriwa kutumia ujuzi walioupata kufanya kazi za ufundi kwa bidii na waaminifu.
Hayo yalisemwa jana na Mjumbe wa Kamati ya Wazazi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam na diwani Mstaafu wa Kata ya Ilala, Edson Fungo kwenye mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
'Kazi za ufundi zinahitaji ujiaminishe mwenyewe kwa sababu kadri fundi unapokuwa mkweli na kutengeneza gari kwa uaminifu ndipo unapoletewa kazi nyingi' alisema Fungo.
Alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita kwenye ujenzi wa viwanda hivyo ametaka vijana waliomaliza mafunzo yao ya ufundi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda lifanikiwe.
Fungo alimpongeza Mkurugenzi Chuo hicho, Bruno Ndege kuanzisha mafunzo ya ufundi na udereva katika eneo la watu maskini la Buguruni ambao vijana wengi ambao hawapati nafasi ya kuendelea na masomo wanajiingiza kwenye vitendo viovu vya wizi na uhalifu.
Alisema Chuo hicho kimekuwa kikisaidia Serikali kuwaandaa vijana kujitegemea na kuwafanya kuwa mafundi stadi wenye uwaledi katika fani hiyo.
Katika risala ya wanachuo hao waliomba serikali iendelee kukaza kamba ya utekelezaji wa kazi iliyoanzisha ya kukagua madereva wasiopitia shule ya udereva ili kupunguza ajali za barabarani.
Mkurugenzi wa BVTC, Ndege alisema kutoka chuo hicho kuanzishwe kimetoa wahitimu 11,041 katika kipindi cha miaka 25 ambao wengi wao wamejiriwa katika sekta mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi.
Alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za utoro wa wanafunzi watukutu na wazazi kushindwa kuwalipia ada watoto wao.
Hivyo makala Mafundi washauriwa kuwa waaminifu
yaani makala yote Mafundi washauriwa kuwa waaminifu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mafundi washauriwa kuwa waaminifu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mafundi-washauriwa-kuwa-waaminifu.html
0 Response to "Mafundi washauriwa kuwa waaminifu"
Post a Comment