BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA .

BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA . - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA ., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA .
kiungo : BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA .

soma pia


BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA .

Mwambawahabari

Mahmoud Ahmad Arusha,
Jumla ya kiasi cha sh,99 bilioni zinatarajia kugharamia ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengeneza dawa za kufubaza virusi vya ukimwi(Arv”s) kinachotarajia kujengwa jijini Arusha.
Kiwanda hicho kinatarajia kuanza kujengwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo kitazalisha jumla ya dawa 500,000 za kufubaza virusi vya ukimwi kwa mwezi na kuwafikia waathirika wa ukimwi milioni moja na nusu nchini kati ya milioni 3 ambao wanaishi na maambukizi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa afisa mtendaji mkuu wa kiwanda cha kutengeneza dawa  nchini(TPH),Ramdhan Madabida alisema kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia kuokoa kiasi cha sh,806 bilioni kwa mwaka zinazotumika serikalini kuagiza dawa nje ya nchi.
Madabida,alisema kwamba fedha za ujenzi wa kiwanda hicho zimetokana na ufadhili walioupata kutoka jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya(EU) ambapo zitatumika katika awamu tatu ambazo ni ukarabati wa majengo,kutengeneza mashine sanjari na kufanya upanuzi wa kiwanda.
Alisema kwamba wao kama wawekezaji wa ndani wameamua kuunga  mkono kauli mbiu ya Rais John Magufuli kuhusu Tanzania ya viwanda na hivyo wamejipanga kutoa ajira kwa vijana nchini zipatazo 200 kwa awamu ya kwanza.
“Mheshimiwa Rais Magufuli ametutia moyo na tuna imani ametupa msukumo sisi tutaendelea na uzalishaji na sio dawa tu pia tutazalisha malighafi na sio dawa pekee”alisema Madabida
Madabida,aliwaambia waandishi wa habari ya kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaendana sanjari na  ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti na maendeleo kwa ajili ya kuboresha utengenezaji wa dawa bora na kukifanya kiwe kitivo cha kutoa taaluma kwa wanataaluma mbalimbali nchini.
Alisema kwamba mashine zote katika kiwanda hicho zitaendeshwa katika teknolojia ya hali ya juu kupitia mfumo wa kompyuta ambapo mbali na kutengeneza dawa hizo za kufubaza virusi vya ukimwi pia kitazalisha dawa za kutibu magonjwa ya vifua,malaria,tumbo sanjari na dawa zilizo kwenye orodha ya dawa muhimu nchini.
“Kuanzia mwaka 2018 tutawekeza katika kuongeza dhana za uzalishaji katika kutengeneza dawa za sindano pamoja na dripu”alisema Madabida


Hivyo makala BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA .

yaani makala yote BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/bilioni-99kugharamia-ujenzi-wa-kiwanda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BILIONI 99,KUGHARAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA ARVS ARUSHA ."

Post a Comment