title : JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake
kiungo : JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake
JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake
JESHI la Wananchi wa Tanzania JWTZ Leo limeadhimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.
Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es salaam chini ya Mkuu wa Majeshi Generali Venance Mabeyo akiwa na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, kwa kufanya usafi katika eneo la kambi ya Jeshi Lugola na baadaye kufuatiwa na michezo iliyofanyika katika eneo la Uwanja wa Jeshi mwenge vinyago .
Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amelipongeza Jeshi hilo kwa kudumisha usafi na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuiga mfano wa Jeshihilo kutumia mazingira kwa usafi na kupanda miti katika maeneoyao.
Aidha Makonda ameelezeakusikitishwa kwake na kitendo cha mgambo wanaosimamia usafi katika jijini la Dar es salaam kwenda kinyume cha sheria katika kusimamia zoezi hilo kwakupiga wananchi na kusema kuwa hajawatuma kufanya hayo na ametoa amri wakamatwe .
''Sheria zipo hakuna hata mmoja inayosema adhabu ya kukutwa na uchafu ni kupigwa bali sheria imeongelea faini, nimeagiza tangu jana walihusika na hilo tukio wakamatwe na hatua za sheria zichukuliwe dhidi yao" alisema.
Kwa upande wake mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wanajeshi kudhibiti usalama wa kambi kwa kutoruhusu raia kukatisha katika maeneo ya Jeshi na kuahidi kujenga ukuta katika eneo la jeshi kambi ya Lugalo na Mwenge na kuhiza usafi kuwa endelevu.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania jenerali,Venance Mabeyo akizungumza viongozi mbalimbali pamoja na wanajeshi la JWTZ katika maazimisho ya miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.
Hivyo makala JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake
yaani makala yote JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/jwtz-laahimisha-miaka-54-tangu.html
0 Response to "JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake"
Post a Comment