title : Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?
kiungo : Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?
Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?
Chimbuko ya bodaboda ni utashi wa wajasiriamali kuvuka mpaka wa Uganda kwenda Kenya, mwaka 1972 - muda mfupi baada ya Idi Amin kuipundua serikali ya Milton Obote katika 1971.
Uhaba wa vitu muhimu majumbani Uganda, uliwafanya wafanyabiashara kutaka usafiri bora wa kuvusha bidhaa kama sukari na chumvi, masafa ya kilomita moja hivi kutoka Kenya, eneo la Busia.
Kama biashara ndogo ya faida, bodaboda inavutia vizito na mabepari kwa mikopo;.Kwa wingi wake, inavutia wenye vyeo na vyama; kwa wepesi wake, inavutia wahalifu.
Kwa hesabu za mwaka 2013, Uganda ilitumia zaidi ya $30m kuagiza pikipiki, siku hizi zinaundiwa nchini.
Huku 70% ya Waganda wakitegemea uchukuzi wa umma, teknolojia ya kurahisha usafiri ikizidi kusasishwa, mustakabali wa bodaboda ni mzuri, licha changamoto za utovu wa sheria barabarani, ajali, na uhalifu.
Tangu bodaboda izinduliwe, kama mfumo wa uchukuzi miaka 47 iliopita, sasa ni ya pili kwa ajira, baada ya kilimo.
Kama kiserema katika kilimo, mwanzo duni wa bodaboda, ulikuwa Baskeli.
Neno Boda Boda limetoka wapi?
Asili ya neno bodaboda, mwasisi wa mfumo huo, Pascali Bwire, anasema, ilikuwa utashi wa wafanyabiashara kuvuka kienyeji masafa ya maili moja, kati ya mpaka wa Uganda na Kenya kwa baskeli, kubeba bidhaa kama sukari, chumvi, unga na sabuni mwaka 1972.
Biashara 'nzuri' wakati huo.
Leo bodaboda ime-sasishwa, toka kengele na magurudmu mawili ya spoki, hadi Pikipiki; na si mpakani tu.Imesambaa mijini na vijijini Uganda. Inakisiwa nusu milioni ziko ndani na kuizunguka Kampala peke yake.
ENDELEA BBC Swahili.
Hivyo makala Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?
yaani makala yote Je unalijua chimbuko la Boda Boda ? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Je unalijua chimbuko la Boda Boda ? mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/je-unalijua-chimbuko-la-boda-boda.html
0 Response to "Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?"
Post a Comment