DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI

DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI
kiungo : DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI

soma pia


DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI

NA Suleiman Msuya,Morogoro 
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe amesema elimu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) ikisambazwa nchini kote misitu itakuwa endelevu na kuepusha nchi kuingia katika jangwa. 

Dk. Kebwe aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) uliofanyika mkoani Morogoro. 

Alisema iwapo elimu ya USM itasambaa kwa kila mwana jamii ni dhahiri rasilimali misitu itakuwa salama kwa muda mrefu hivyo ni imani yake kila kiongozi atatoa kipambele. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema uhifadhi misitu ni jambo ambalo haliepukiki hasa katika kipindi hiki kwa kuwa madhara yakutohifadhi yameshaonekana jwa sasa. 

“Napenda kutumia nafasi hii kuziomba mamlaka husika ili elimu ya USM ifikie kila kiongozi katika nchi kwani takwimu za kuharibiwa kwa hekta 469,000 kila mwaka ni dalili za jangwa na Morogoro pekee inaharibu hekta 150,000 sawa na asilimia 48 ya uharibifu wote,” alisema. 

Alisema iwapo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) itaweka taratibu ambazo zitaelekeza njia mbadala ya kukabiliana na uvunaji wa miti kwa sababu ya kaa hali itakuwa salama. 

Dk. Kebwe alisema kinachoonekana kwa sasa ni kukosekana kwa maelekezo sahihi ambayo yatasababisha sheria kusimamiwa kikamilifu. 

Alisema katika mkoa wake atahakikisha wasaidizi wake wanasimamia rasilimali misitu kwa weledi huku ikifaidisha jamii zaidi ambayo inazungukwa na misitu hiyo. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo kila mkoa utatembea na dhana ya kuhakikisha jamii inanufaika na rasilimali hiyo ni wazi kuwa ulinzi utakuwepo na dhana ya uchumi wa viwanda itaonekana moja kwa moja. 

Mwenyekiti wa Mjumita Taifa, Revocatus Njau alisema wao wamejikita katika kutoa elimu ya usimamizi shiriki wa misitu baada ya kugundua jamii kubwa haina uelewa. 

Njau alisema pamoja na elimu pia wanahakikisha jamii inamiliki misitu inanufaika nayo kwa kufanya shughuli za kiuchumi kwa kufuata sheria za nchi. 

“Kwa miaka 18 tumekuwa tukitoa elimu ya utunzaji na unufaikaji kupitia rasilimali misitu, ila ipo changamoto kwa baadhi ya watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na waharibifu wa misitu hali ambayo inatudisha nyuma,” alisema. 

Kwa upande wake Ofisa Misitu Mwandamizi kutoka Tamisemi Rogasian Lukoa alisema Serikali inajipanga kuhakikisha elimu ya USM inasambaa kwa kila mwanajamii ili kuwa mlinzi sahihi wa rasilimali hiyo. 

Lukoa aliwataka watendaji wa Serikali kuanzia ngazi za vijiji kushirikiana na taasisi kama Mjumita, Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Jamii Tanzania (TFCG) na wengine ili kuhakikisha misitu inakuwa endelevu.


Hivyo makala DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI

yaani makala yote DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dkkebwe-ataka-elimu-ya-usm-isambazwe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI"

Post a Comment