title : MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32
kiungo : MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32
MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32
KATIKA hali isiyoya kawaida kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambacho kwa wiki iliyopita madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) walisusia kikao hicho mstahiki meya Alex Kimbe amewashangaza wengi baada ya kuendesha kikao kwa dakika 32 na kugoma kusikiliza hoja binafsi .
Kikao hicho kilianza saa 2.00 hadi saa 2.32 huku madiwani takribani 10 wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) wakiwa na ukumbini na CCM akiwemo diwani mmoja pekee na naibu meya Joseph Lyata kiliweza kuendeshwa kwa aina yake baada ya mstahiki meya kufungua kikao hicho kwa sala baada ya hapo kuwaita bila kutokea wajumbe watatu wawili wa CCM na mmoja wa Chadema kuuliza maswali ya papo kwa papo kwa meya .
Kutokana na wajumbe hao wa kikao kutokuwepo alifunga zoezi hilo na kuendelea na agenda nyingine za kikao ikiwa ni pamoja na kusoma taarifa za kamati mbali mbali na kuruhusu wenye maswali juu ya kamati hizo kuuliza maswali baada ya hapo alitangaza kuzikataa hoja binafsi ambazo takribani tatu ambazo zilikuwepo kwa madai ya kutozingatia kanuni za baraza hilo kwa hoja hizo kufikishwa kwa maandishi kabla ya kuletwa katika baraza .
" Ndugu wajumbe kwa kuwa hakuna hoja binasi zilizopo ni za mdomo tuu naomba kumkaribisha katibu wa kikao kwa maneno machache na baada ya hapo nifunge kikao chetu " alisema meya Kimbe .
Kuwa anawashukuru wajumbe waliofika kwa wakati katika kikao hicho ambacho kimsingi kilitangazwa kuanza saa 2 .00 asubuhi hivyo wajumbe waliochelewa wamechelewa kikao hicho alisema na kutangaza kufunga kikao huku baadhi ya madiwani wakiendelea kuwasili ukumbini .
Wakizungumza mara baada ya kikao hicho aliyekuwa meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi (CCM) alisema anashangazwa na hatua ya kikao kumalizika kwa muda mufupi wakati kulikuwa na hoja za msingi hasa kwenye kamati ya mazingira juu ya eneo la Kihesa Kilolo eneo la uwekezaji ambalo waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na waziri wa TAMISEMI walishauri eneo hilo kutojengwa viwanja vya michezo na badala yake kujenga vitega uchumi kama ukumbi wa mikutano wa AICC .
lla alisema anashangazwa kuona anapingwa na meya na kuwa hoja hiyo haina nafasi katika kikao hicho na badala yake kuzuia kujadiliwa na kukimbilia kufunga kikao .
Hivyo makala MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32
yaani makala yote MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/meya-iringa-awashangaza-madiwani.html
0 Response to "MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32"
Post a Comment