title : AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA
kiungo : AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA
AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA
Ikiwa imepita miezi miwili tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuagiza pikipiki zote zinazotumika kusafirisha abiria zifungwe tela katika kile kinachoaminika kudhibiti wimbi la ajali za bodaboda,Taasisi mbalimbali za Serikali zimekutana jijini Dodoma ikiwa ni mazungumzo ya awali kuelekea mkakati huo wa kupunguza ajali.
Akizungumza jijini Dodoma baada ya mkutano na ukaguzi wa pikipiki ya mfano iliyofungwa tela iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga,lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Serikali imedhamiria kuondoa na kukomesha ajali za bodaboda pamoja na kulinda usalama wa watumiaji wa usafiri huo.
Akielzezea juu ya mazungumzo hayo yaliyokutanisha taasisi hizo, Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Wizara yake kwa kushirikiana na wadau wengine kutoka taasisi za serikali; Shirika la Mzinga, Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Kiwanda cha Kutengeneza Magari (NYUMBU) na Jeshi la Polisi watahakikisha wanakuwa na mpango wa pamoja wa kuratibu na kuhakikisha mkakati huo utakaosaidia kupunguza ajali unakamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(aliyepanda pikipiki), akisikiliza maelezo ya kiufundi kutoka kwa mmoja wa wataalamu kutoka Shirika la Mzinga, Whemy Lyimo(kulia) waliotengeneza pikipiki hiyo yenye tela ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri, Kushoto ni dereva wa pikipiki hiyo,Stanley MsuyaTukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Taasisi za Serikali baada ya kukagua Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
Hivyo makala AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA
yaani makala yote AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/agizo-la-waziri-lugola-laanza.html
0 Response to "AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA"
Post a Comment