title : MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA
kiungo : MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA
MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA
Na. Honorius Mpangala.
Southampton ni moja ya klabu ambayo inaaminika kuwa na shule nzuri ya soka. Kuaminika huko kunatokana na matunda yaliyotokana na shule hiyo katika kukuza soka la vijana.
Katika klabu Southampton ndiko walikopita vijana kama Theo Walcott,Alex Oxlade-Chamberlain,Gareth Bale,Adam Lallana,Luke Shaw,Calum Chambers. Imani hiyo ya uwepo wa shule bora inatokana na uwezo wa vijana wanaoibuaka katika klabu Hiyo na kuhitajika sana wakati sa soko la usajili kwa wachezaji.
Licha ya kuwa na mmiliki mwanamke Katharina Liebherr,klabu hiyo imeweza kuimarika katika ufanyaji wa biashara na
Kuhimili katika ligi kwa maana ya kutumia rasilimali zao ndani ya klabu.
Uwezo wa kasi aliyokuwa nayo Bale,Walcott na Chamberlain umetoka katika shule ya Southampton. Baada ya kufanya vyema katika klabu hiyo Ilikuwa ni Tottenham Hotspur waliamua kumsajili Bale. Wakati bale anasajiliwa ilikuwa tayari Arsenal walishamsajili Walcott.
Bale alipofika katika klabu ya Tottenham alisajiliwa kama mlinzi wa kushoto.Alifanya vyema sana katika nafasi hiyo akiwa chini ya kocha Harry Rednap. Unaweza kusema Majeruhi ya nyota hufanikisha kumtoa kinda au kutoa nafasi kwa mchezaji mwenza katika nafasi moja.
Baada ya Bale kupata majeraha na kumweka nje kwa ya kikosi cha Tottenham,nafasi yake ilichukuliwa na Benoit Assou-Ekotto. Mkameruni huyo aliitendea vyema nafasi ile ya mlinzi wa kushoto kiasi kwamba ilitia shaka endapo Bale angelejea.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kurejea kwa Bale kulimfanya Rednap amtumie kama Kiungo wa pembeni kushoto. Bale alifanya vyema katika nafasi hiyo huku ile ya mlinzi ikikabidhiwa moja kwa moja kwa Ekotto.
Bale wa leo ni matokeo ya kiwango bora cha Ekotto kilichomfanya Kocha ambadilishe nafasi. Maamuzi ya Rednap ndiyo yaliyofanya Bale aje kununuliwa kwa kiasi cha pesa cha paundi milioni 85 kwenda Real Madrid.
Katika klabu ya Yanga kuna Gadiel Michael ambaye kwasasa amekuwa mlinzi bora kwa klabu na timu ya taifa.Kwa kipindi hiki ambacho Yanga wamepungua makali katika maeneo yao ya winga kulia na kushoto ingekuwa kamari nzuri endapo Mwalimu George Lwandamina angejaribu kumchezesha Gadiel kama winga na Nafasi ya ulinzi ikarejea kwa Mwinyi Haji Mngwali.
Hivyo makala MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA
yaani makala yote MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/makala-michezo-gadiel-michael-anaweza.html
0 Response to "MAKALA MICHEZO: GADIEL MICHAEL ANAWEZA KUWA MSAADA WA NAFASI YA WINGA YANGA"
Post a Comment