title : ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA.
kiungo : ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA.
ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA.
Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Makampuni matano kutoka Korea Kusini na China wameonesha nia ya Uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba hapa nchini.
Makampuni hayo matano wameonyesha nia ya kuwekeza baada ya kufanyika ziara ya Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) nchini Korea Kusini, huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alishiriki kongamano la biashara na uwekezaji liliofanyika China Agost I6 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe, amesema kuwa kupitia ziara ya kikazi aliyofanya mwezi huu nchini Korea kusini wamefanikiwa kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini.
Mwambe amesema kuwa katika ziara hiyo walishiriki kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika Agosti I3 mwaka huu korea kusini ambapo wafanyabiashara walijadili fursa za Uwekezaji katika sekta ya madawa na vifaa tiba.
Ameeleza kuwa ili kufanikisha ufanisi katika ziara hiyo aliongozana na wawakikishi wa taasisi za serikali, Makapuni binafsi, Viongozi wa Chama Cha Watengenezaji na Wauzaji wa Madawa (TAPI).
"Makongamano haya yaliambatana na ziara za kutembelea viwanda vinavyomilikiwa na baadhi ya makampuni yalionesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania" amesema Mwambe.
Ameeleza kuwa katika ziara hizo kulisainiwa hati za maafikiano (MOU) tatu kati ya TAPI na wafanyakazi wa makampuni ya China ili kuwezesha mafanikio na makampuni ya Tanzania kuwekeza kwa ubia katika sekta ya Afya.
"Lengo la kushiriki magongamano hayo ni kuleta mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania" amesema Mwambe.
Katika hatua nyengine Mwambe amefafanua kuwa Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kufanya kuboresha huduma za mahali pamoja (One stop facilitation Centre) ili kuwahudumia wawekezaji kwa ufanisi mkubwa.
Amesema kuwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imejumuika na taasisi nyingine za serikali ambazo tayari zipo TIC ili kudumisha wawekezaji.
Katika kutengeneza Mazingira rafiki kwa wawekezaji taasisi zote ambazo zinafanya kazi kwa ukaribu na TIC ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikwa na kupiga hatua katika masula mbalimbali ya maendeleo.
Hivyo makala ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA.
yaani makala yote ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/ziara-ya-mkurugenzi-tic-korea-kusini.html
0 Response to "ZIARA YA MKURUGENZI TIC KOREA KUSINI YALETA NEEMA YA WAWEKEZAJI TANZANIA."
Post a Comment