title : SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
kiungo : SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
Na.Mwandishi Maalum.
Katika moja ya jitihada za kuhakikisha mafanikio ya mkakati wa kujenga Uchumi wa Viwanda nchini serikali imeendelea Kuboresha mazingira bora ya biashara kwa wawekezaji kwa kuendeleza kilimo ili kuchochea maendeleo na sekta ya kilimo kupitia Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Akizungumza baada ziara ya Kukagua shughuli za SAGCOT mkoani Iringa kwa kutembelea kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Silverlands na kiwanda cha kusindika Maziwa cha Asas Diary Milk, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora alifafanua kuwa njia ya kuliwezesha Taifa kuwa na uchumi imara utakaohimili ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa ni kuboresha mazingira ya Uwekezaji.
“Tunaweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa kiuchumi katika sekta ya kilimo hasa kwa kuishirikisha sekta binafsi na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, tunao Mpango wa SAGCOT tunataka kutumia fursa hizi katika kilimo kukuza uchumi, tuondokane na kilimo cha kujikimu na kuhamia kilimo biashara. Wawekezaji wanahitaji kuona utayari wa wakulima ili wawekeze. Tukumbuke zaidi ya asilimia 70 ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo”, alisema Kamuzora.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ,Wamoja Ayoub, alifafanua kuwa tayari mkoa huo umeanza kupata mafanikio kwa utekelezaji wa SAGCOT mkoani humo kwa wakulima kuweza kulimochenye tija , kuongeza thamani mazao yao na kupata masoko ya uhakika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifurahia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, wengine ni Mkurugenzi wa Mashamba na Mifugo Kiwanda cha, Rob Nethersole na Mratibu wa SAGCOT Ofisi ya Waziri Mkuu, Girson Ntimba.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj, wakati alipofanya ziara mkoani Iringa, kukagua viwanda vinavyofanya kazi na Kongani ya Ihemi inayotekelezwa na Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/serikali-kuendelea-kuboresha-mazingira_24.html
0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI"
Post a Comment