WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI

WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI
kiungo : WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI

soma pia


WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI

Baadhi ya wafugaji wilayani Rungwe wameitaka Kampuni ya Asas inayojihusisha na ununuzi maziwa wilayani humo, kuhakikisha inajenga kiwanda ili maziwa yaongezewe thamani na kuuzwa kutokea wilayani humo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani humo, wamesema kitendo cha Asas kuweka kituo cha kukusanyia maziwa wilayani Rungwe na kuyasafirisha kwenda kiwandani Mkoani Iringa, kinasababisha wanunue maziwa kwao kwa bei ya chini ili kufidia gharama nyinginezo ikiwemo usafirishaji tofauti kama wangekuwa na kiwanda.
Mfugaji wa kijiji cha Syukula kata ya Kyimo wilayani humo, Mabua Mwakalimbila alisema bei wanayouza maziwa kwa lita moja ipo chini, hailingani na gharama wanazotumia kumuhudumia ng'ombe hadi kufikia hatua ya kutoa maziwa.
"Wangekuwa wananunua kwa Sh 1,000 kwa lita ingekuwa ni nafuu, lakini kwa Sh 600 ni fedha kidogo, lakini naamini wakijenga kiwanda hapa gharama wanazotumia kukusanya maziwa na kuyasafirisha zitapungua hivyo wataongeza bei katika ununuzi wa maziwa,"amesema.
Joseph Mafundo amesema ikiwa kampuni ya Asas itashindwa kujenga kiwanda wanatamani idadi ya wanunuzi iongezeke ili kuwe na ushindani katika ununuzi.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Asas, Ben Mwakanyamale alisema kampuni hiyo imeteua kata sita za mfano ambazo wanatoa elimu ya ugani kwa wafugaji kwa kushirikiana na serikali.
Wanakusudia kujenga kituo cha kukusanyia maziwa katika kila kata ili kuwapunguzia wafugaji gharama za usafirishaji wa maziwa.
Amezitaja kata hizo kuwa ni Kiwira, Malindo, Lufingo, Ipogolo, Nkunga na Kyimo na kwamba wanakusudia kujenga kiwanda wilayani Rungwe ili kuongeza thamani ya maziwa na kuchochea ongezeko la ajira na kukuza pato la wilaya.
Ukosefu wa soko la uhakika la maziwa wilayani Rungwe unadaiwa kusababisha upotevu wa lita zaidi ya milioni 50 kwa mwaka kati ya lita zaidi 60 milioni zinazolishwa kwa mwaka wilayani humo, ambapo kwa takwimu hizo inakadiriliwa lita 200,000 hupotea kati ya 230,000 zinazolishwa kwa siku.


Hivyo makala WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI

yaani makala yote WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wafugaji-wataka-kiwanda-kuongeza-thamani.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAFUGAJI WATAKA KIWANDA KUONGEZA THAMANI"

Post a Comment