TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA.

TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA.
kiungo : TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA.

soma pia


TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA.

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeipongeza Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) kwa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa malengo ya ubinafsishaji na kuendeleza azma ya serikali ya viwanda.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyoratibiwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na pia kuhudhuriwa na Naibu Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya na watendaji wengine kutoka wizara hiyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Sadiq`Murad' ameipongeza TCC Plc kwa mafanikio hadi sasa na kuongezea kuwa kamati yake iliridhishwa na walichokiona na kuutaka uongozi na wafanyakazi kuendeleza kazi hiyo nzuri.
“TCC Plc ni mfano mzuri wa kweli unaopaswa kuigwa kwa wengine kwani utatambua imekuwa imara katika ulipaji wa kodi serekalini.. Kamati yangu imezichukua changamoto zao na tutaishauri serikali inavyostahili ili kuhakikisha wawekezaji kama TCC Plc wanafanya shughuli zao bila wasiwasi,” amesema.
Mwenyekiti huyo pia aliipongeza TCC Plc kwa kukuza vipaji vya ndani kwani hadi sasa kuna wakurugenzi watano wa kitanzania katika Menejimenti ya Juu inayoundwa na wakurugenzi wanane.
Hivi karibuni kampuni hiyo imeshuhudia uteuzi wa Sam Mandara kama Mkurugenzi wa uzalishaji ambaye ni mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kampuni hiyo ibinafsishwe.
Manyanya alisema TCC Plc imekuwa mfano wa kweli katika mafanikio ya ubinafsishaji kwani mashirika mengine yaliyobinafsishwa wakati mmoja na TCC Plc yalishindwa kujiendesha na yamekufa wakati kampuni hiyo imeendelea kukua na kujiendesha kwa faida miaka yote.
Aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwekeza katika nishati ya umeme wa gesi kwani hatua hiyo haijahakikisha tu gesi inayozalishwa nchini inatumika, bali pia imehakikisha wakazi wa maeneo ya Chang’ombe, Temeke hawapati adha za mgawo wa umeme, kwani kampuni hiyo haitumii umeme mwingi kutoka kwenye gridi ya taifa.
Meneja Mkuu na Mtendaji Mkuu wa TCC Plc, Allan Jackson ameishukuru kamati hiyo kwa kuwa bega kwa bega nao hadi sasa ambapo imeiwezesha TCC Plc kufikia malengo yake tangu kuanzishwa kwake.
Aliongeza kusema kwa mwaka jana pekee TCC Plc ililipa serikalini kodi ya ongezeko la thamani (VAT), mapato na ushuru wa bidhaa kiasi cha Sh bilioni 227, jambo ambalo wabunge wanatakiwa kujivunia.
Aliwakumbusha wabunge kuwa TCC Plc ni mali ya watanzania na kuwa yeye na wafanyakazi ni wasimamizi tu kwa niaba ya wanahisa wa kampuni hiyo.


Hivyo makala TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA.

yaani makala yote TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tcc-yapongezwa-utekelezaji-sera-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TCC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI SERA YA VIWANDA."

Post a Comment