title : TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI
kiungo : TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI
TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI
Na.Vero Ignatus -Arusha
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya uthibiti wa viasilia vya mionzi vinavyoweza kupatikana kwenye mazao ya chakula na mifugo ili kuongeza usalama wa mtumiaji dhidi ya madhara hatari yanayosababishwa na mionzi.
Katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini wanatoa elimu juu ya nyuklia inayoweza kuwa mkombozi kwenye ukuaji wa uchumi wa biashara na viwanda ikilenga matumizi salama teknolojia nchini ili kuboresha ustawi wa kwenye sekta ya afya,maji ,kilimo,nishati na mifugo.
Mtafiti wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Yesaya Sungita amesema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30%ya vyakula duniani vinahribika kila mwaka kwa sababu ya kuharibiwa na na vijidudu au kuoza ,upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato cha wakulima.
Aidha kila mwaka inakadiriwa hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika haswa kusini mwa jingo la sahara inafikia dola za kimarekani bilioni 4 sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayosambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella yanafikia iddi ya watu 120,000 kila mwaka ambapo maambukizi yamekuwa yakisbabisha vifo vingi.
"Gharama ya matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu vya salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni 6 kila mwaka.alisema Yesaya"
Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Yesaye Sungita, wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo akiguatiwa na Mtafiti wa Tume hiyo Jerome Mwimanzi wakitoa elimu kwa mmoja wa mgeni aliyetembelea katika banda hilo katika maonyesho ya nane nane Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro Arusha.
Hivyo makala TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI
yaani makala yote TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tume-ya-nguvu-ya-atomiki-nchini-yatoa.html
0 Response to "TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI YATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI"
Post a Comment