title : TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA
kiungo : TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA
TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameendelea na ziara yake katika ukanda wa ziwa Viktoria katika kugagua na kuangalia utekelezaji wa sekta hiyo.
Baada ya malalamiko ya wavuvi kuhusiana na nyavu hasa za dagaa wamejiridhisha kuwa na tatizo na wametoa idhini ya uingizaji wa nyavu nchini ili kumaliza tatizo hilo.
Ulega ameeleza kuwa nyavu chini ya milimita nane kutumika kuvulia dagaa ni shida na haikubaliki na zile zenye macho ya inchi 26 zinafaa zaidi.
Kuhusu ukataji wa leseni Ulega amesema kuwa wasiofuata taratibu lazima wakamatwe na wafanyabiashara wote lazima wawe na vibali maalumu vya kufanya shughuli za uvuvi.
Aidha amesema kuwa wana maboresho ya sheria na kanuni za uvuvi na kodi ili wafanyao shughuli hizo kuwa na uwezo wa kutambua shughuli wanazozifanya.
Kuhusu kuingiza nyavu haramu Ulega amesema kuwa wamejipanga na watachukua hatua kwa wale wote watakaokiuka kanuni na sheria katika kuhakikisha sekta hiyo inakwenda mbele na Wizara hiyo haina tatizo na watu watakaofata sheria.
Makabidhiano hayo kuwakabidhi wafanyabiasharavibali vya kuagiza nyavu nchini yamefanyika katika mpaka wa Tanzania na kenya Sirari.
Wafanyabiashara hao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia vibali vya kuingiza zana hizo na wamehaidi kufanya kazi kwa kufuata sheria kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.
Naye Meneja wa kiwanda cha Musoma Fish, George Fernandez ameishukuru sana Serikali kwa kuendelea na kupambana na uvuvi haramu kwa sasa samaki wanapatika kwa wingi na amesema kiwanda hicho kinafata sheria ya kutokuchakata samaki ambao sheria haiwatambui na wanalipa kodi kulingana na sheria inayo waelekeza ili kuongeza mapato kwa Serikali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alimkabidhi mfanya biashara,Majani Masangati kibari cha kuingiza nyavu za Uvuvi nchini ambapo amewaomba wanyabiasha ote waingize zana hozo kwa kufata sheria za nchi.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Musoma, John Kayombo na viongozi wengine wakikagua uzalishaji wa kiwanda cha samaki Musoma Fish.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akisalimiana na Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Musoma,John Lipesi Kayombo marabaadaya kuwasiri mkoa wa mkoa wa Mara.
Hivyo makala TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA
yaani makala yote TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tatizo-la-nyavu-kwa-wavuvi-ziwa.html
0 Response to "TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA"
Post a Comment