title : MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA
kiungo : MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA
MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA
*Ni ishara ya kumuombea dua kwa Mungu,pia kumshukuru kwa kusaidia kutatua kilio chao
MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali ameamua kumshika kichwa mdau wa maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.
Pia ikiwa ni kumshukuru baada ya kufanikisha familia hiyo na nyingine zaidi ya tano kijijini hapo kulipwa fidia ya mashamba yao yaliyokuwa yamechukuliwa na mkandarasi wakati wa ujenzi wa barabara ya Dodoma - Babati.
Imeelezwa kuwa wananchi hao walikata tamaa mwishoni mwa mwaka juzi kutokana na kufuatilia malipo yao bila mafanikio. Hivyo Mkotya aliguswa na kero hiyo hivyo aliamua kushirikiana nao na kuwapigania hadi walipolipwa stahiki zao.
Juzi wakati Mkotya akitoka Dodoma kwenda Kondoa aliamua kupita kijijini hapo ndipo familia hiyo ilipomkaribisha nyumbani ili aone matunda ya kazi yake ya kuwapigania.
Familia hiyo ilimweleza Mkotya kuwa inayofuraha kubwa kwani fedha walizopata wameweza kununua mashamba mengine na kujenga nyumba bora ya bati.
MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali akiwa amemshika kichwa mdau wa maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.
Mdau wa Maendeleo wilaya ya Chemba,Hamis Mkotya akizungumza jambo na Mkazi wa kijiji cha Kidoka Wilayani Chemba,Roza Mkali hivi karibuni mara baada ya tatizo walilokuwa nalo kutatuliwa
Hivyo makala MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA
yaani makala yote MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkazi-walayani-chemba-amshika-kichwa.html
0 Response to "MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA"
Post a Comment