title : MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU
kiungo : MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU
MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amejitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana katika Hospital hiyo ya kibingwa wakati akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu.
Kutokana na changamoto hizo zinazomkabili mtoto Christopher, Naibu Waziri Mavunde akishirikiana na Mbunge wa Bahi Mh Omary Badwell wameahidi kumsaidia miguu ya bandia miwili na pia kumsomesha katika shule ya Fountain Gate Medium School iliyopo Miyuji Jijini Dodoma ili kumsaidia mtoto kutimiza ndoto zake za kielimu na maisha kwa ujumla.
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dr Alphonce Chandika alisema Hospital imeona imsaidie mtoto Christopher kiti hicho cha kutembelea ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwajali na kuwasaidia watanzania wenye vipato vya chini.
"Kweli tumeokoa maisha ya Christopher tena bila kumtoza gharama, lakini tusingeishia hapo kwasababu tayari ni mhitaji, hivyo tumempatia kiti hiki na sasa tunawaomba watanzania wamsaidie miguu bandia, suala elimu na mahitaji mengine muhimu ili ajimudu katika maisha yake" alisema Dkt Chandika.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu kujitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.
Naibu Waziri Mavunde akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu.

Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano.
Hivyo makala MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU
yaani makala yote MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mavunde-ajitolea-kumsomesha-na-kumlea.html
0 Response to "MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU"
Post a Comment