title : KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI
kiungo : KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI
KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI
KATIBU tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi ametembelea katika kijiji cha Hamai kukagua ujenzi wa zahanati ya Hamai inayojengwa na wananchi wa kijiji hicho na kusikiliza changamoto zao, pia ametoa vifaa vya ujenzi na kushiriki kufanya baadhi ya kazi za ujenzi wa zahanati hiyo.
Akizungumza na Mafundi ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai amesema kuwa zahanati hiyo inatakiwa imalizike kwa haraka na kwa ufanisi mzuri ili kusaidia wananchi kupunguza kilometa za kutembea kwaajili ya kutafuta huduma mhimu ya kijamii ya afya.
Pia wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji amewaongezea wahandisi wa ujenzi na kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi ambavyo ni Mbao, misumari chokaa pamoja na tiles.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi ametoa vifaa vya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma vifaa hivyo ni pamoja na mbao, tiles chokaa na misumari.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akitembelea ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akisaidia kupaka rangi kwenye jengo la zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akizungumza na wajenzi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma mara baada ya kutoa mchango wa vifaa ya ujenzi pamoja na kuwaongezea wahandisi wa ujenzi kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la zahanati.
Hivyo makala KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI
yaani makala yote KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/katibu-tawala-wa-wilaya-ya-chemba.html
0 Response to "KATIBU TAWALA WA WILAYA YA CHEMBA ATEMBELEA UJENZI WA ZAHANATI YA JIJINI CHA HAMAI"
Post a Comment