title : HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA
kiungo : HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA
HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA
SAA 2:05 ya asubuhi ya jana ya Agosti 4 mwaka 2018 nilituma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa Ofisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Hamza Temba.
Nakumbuka ujumbe huo niliutuma saa 2:05.Nikiri nimekuwa na na kawaida ya kuwasiliana mara kwa mara na Temba.Hivyo baada ya kuona kuna taarifa inasambaa mtandaoni kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala kupata ajali mkoani Manyara na hali yake ni mbaya sana.
Nikaamini mwenye majibu sahihi kuhusu taarifa ya Waziri kupata ajali atakuwa Temba.Basi nikachukua simu yangu na kuanza kupiga.Mara ya kwanza ikaaita bila kupokelewa.Nikapiga mara ya pili pia haikupokelewa. Nikapiga tena mara ya tatu nayo ikawa haina wa kuipokea.
Hivyo nakaona ngoja nitumie ujumbe mfupi wa simu. Ujumbe niliomuandika ulisema hivi "Kaka habari za asubuhi, nakutafuta plz".Ni jumbe ambao niliamini akiona basi lazima tutawasiliana.Kinachonisikitisha kumbe wakati namtumia ujumbe huo Hamnza Temba pumzi yake ilishakata.Macho yake yalishafumba. Temba kumbe alikuwa ameshalala na hataamka tena.Hakuna na uwezo wa kujibu ujumbe wa simu yangu tena.
Kwangu ni ujumbe ambao kwa mara ya kwanza nauandika kwa Temba lakini haukupata nafasi ya kujibu na hautajibiwa tena.Kwa kifupi Hamza Temba hatunaye tena.Amefariki dunia jana asubuhi mkoani Manyara baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali.
Temba alikuwa pamoja na Waziri Dk.Kigwangala ambaye amejeruhiwa na sasa anaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili.Kifo cha Temba kimeniuma sana.Ni kijana aliyeijua vema kazi yake.Hamza Temba ni Ofisa Habari wa Wizara aliyekuwa na nidhamu kwa kila mtu.Upendo , upole na ucheshi wake hauna mfano.Hakika Temba alikuwa Ofisa wa Habari wa Wizara anayejua kuishi na waandishi wa habari.
Ni ofisa habari wa wizara mwenye heshima ya hali ya ju.Hakuwa na dharau hata kidogo.Moja ya tatizo ambalo ninalo mimi binafsi ni kwamba mtu anapofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake huwa siwezi kuficha lazima niamwambia.Juni mwaka huu niliamua kumpigia simu Temba na mazungumzo yangu yalijikita katika kumpongeza na kumsifu kwa namna ambavyo anatekeleza majukumu yake.
Hivyo makala HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA
yaani makala yote HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/hamza-temba-umeondoka-bila-kujibu.html
0 Response to "HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA"
Post a Comment