title : SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR
kiungo : SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR
SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV, Bukoba.
Timu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imewasili salama katika Manispaa ya Bukoba mapema Ijumaa Aprili 19, 2019 tayari kwa Mchezo wao na Wenyeji Timu ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Kaitba.
Baada ya Kupokelewa na mashabiki ndakindaki na wanazi pamoja na viongozi wa matawi ya Kalbu hiyo,majira ya saa nne asubuhi Uwanja wa ndege wa Bukoba, Timu ya Simba Imesindikizwa kwa msafara wa magari na bodaboda hadi hotelini (STELLA HOTEL) maeneo ya Kashura ambapo Klabu hiyo itakuwa hapo kwa mapumziko na baadae itafanya mazoezi mepesi Uwanjani kaitaba majira ya mchana.
Mchezo wa kesho Kati ya Simba na wenyeji Kagera Sugar ni mchezo wa 152 mzunguko wa kwanza (kiporo) mchezo ambao ni muhimu sana kwa Timu zote mbili wakati Simba ikiwa katika mbio za Ushindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagera wao wakiwa mbioni kutetea nafasi ya kutoshuka daraja, kwani kwa mechi sita zilizosalia Timu hii ya Kagera Sugar inatakiwa kuvuna pointi sita ili isiweze kushuka daraja.
Waamuzi wa mtanange huo hapo kesho, ni pamoja na Jacobo Adongo (Mara), Ferdinand Chaha (Mwanza), Joseph Matija (Mwanza), na Ahmada (Kagera).
Shabiki wa Kagera Sugar, akikatiza mitaa mbalimbali ya Bukoba Manispaa kuwapa hamasa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kuipa nguvu watapopepetuana na Simba leo uwanja wa Kaitaba
Shabiki wa Simba Bi Rehema Ngelekule akiongea na Michuzi TV juu ya mtanange huo
Mtoto Eligius Erasto (6) anasema kajiandaa vyema kuishangilia timu yake
Simba wakiwasili Bukoba
Mshambuliaji Meddie Kagere na mshabiki wa Simba Eligius
Mashabiki wa Simba wakisindikiza basi la wachezaji kuelekea Stella Hotel
Mashabiki wa Simba wakisindikiza basi la wachezaji kuelekea Stella Hotel
Mashabiki wakiwa wamejipanga maeneo ya Kashura ilipo Stell Hotel
Msafara wa Simba wakielekea mazoezini uwanja wa Kaitaba
Wachezaji wa Simba wakiwa uwanja wa Kaitaba wakijiandaa tayari kwa mtanange wao na Kagera Sugar leo jioni

Hivyo makala SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR
yaani makala yote SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/simba-wawasili-bukoba-tayari-kwa-mechi.html
0 Response to "SIMBA WAWASILI BUKOBA TAYARI KWA MECHI YAO NA KAGERA SUGAR"
Post a Comment