title : DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato
kiungo : DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato
DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato
Mwambawahabari
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kukusanya mapato ya halmashauri.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema aliyasema hayo Mkoani Morogoro katika kilele cha sikukuku ya Wakulima nanenane ambapo halmashauri ya Ilala imeshika nafasi ya tatu katika maonesho hayo ya 25 ya Wakulima .
"Nawaomba Watendaji wa halmashauri yangu muda wa kukaa ofisini kwa sasa umekwisha badala yake kila mtu afanye kazi tuweze kukusanya mapato yetu "alisema Mjema.
Alisema tutakapofatilia ukusanyaji wa mapato yetu pato letu la Ilala litakuwa tutaibua miradi mingi ya Maendeleo kwa manufaa ya wananchi wetu.
Alisema tutakapokusanya mapato ya kutosha uchumi wa Ilala utakuwa itaibuliwa miradi mingi .
Aliwataka watendaji wote kuwajibika kila mwenye idara yake kusimamia misingi ya kazi yake na kufanya kazi kwa weledi.
"nawaomba tufanye kazi pia tufatilie mapato tunapokuwa na mapato ya kutosha kila kitu kitakuwa sawa, tutajenga Shule zetu tutaboresha huduma za Afya na kuibua miradi "alisema
.
Akizungumzia ushindi wa nafasi ya tatu katika maonesho hayo 25. ya Wakulima Kanda MASHARIKI Nanenane Morogoro alisema atajipanga vizuri na Watendaji wake wa Idara ya Kilimo pale walipokosea ili mashindano yajayo washike nafasi ya kwanza wataboresha na kuja na ubunifu Mpya katika sekta ya kilimo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ilala Palela Msongela alisema wameyapokea maagizo ya Mkuu wa wilaya ya Ilala watatekeleza.
Alisema atakaa na Watendaji wake na kuyafanyia kazi kila mkuu wa idara aweze kusimamia majukumu yake ili kwenda na kasi ya hapa Kazi Tuu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM WILAYA ILALA Ubaya Chuma alisema ilipo Serikali chama cha Mapinduzi Kipo Wilaya ya Ilala watashirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala katika kutatua changamoto za Ilala na utekelezaji wa ilani.
Hivyo makala DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato
yaani makala yote DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dc-ilala-ataka-watendaji-ilala.html
0 Response to "DC Ilala ataka watendaji Ilala kukusanya mapato"
Post a Comment