Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka

Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka
kiungo : Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka

soma pia


Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Balozi  wa  Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia),  juu  ya  kubadilishana  uzoefu katika Udhibiti  wa  Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam
Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  juu ya kubadilishana  uzoefu  katika  Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi  Ndogo  ya  wizara, jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiagana na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo  hayo  yamefanyika  leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Tanzania na Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa yote nchini iliyopo mipakani
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa ya mipakani
“Kama Serikali tuna vipaumbele katika kudhibiti  mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu huo”alisema Masauni
Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti  wa mipaka.
“Tuna uhusiano mzuri baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak
Katika mazungumzo hayo pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika shughuli za uokozi.


Hivyo makala Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka

yaani makala yote Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tanzania-na-kuwait-zajadili-udhibiti-wa_8.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka"

Post a Comment