title : Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha
kiungo : Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha
Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha
Timu ya mashabiki na wanachama wa Yanga inayofahamika kama Yanga Fb Fans imeichapa mabao 6-4 timu ya wadau wa kandanda, Kandanda Fc, katika mchezo ambao mkali ulioombwa na Yanga kupitia app ya Spocha. Mchezo huu ulifanyika katika kiwanja Posta Kijitonyama siku ya Jumapili.
Spocha ni App ambayo ipo katika majaribio ya awali, ambayo kwa sasa inalenga kuzikutanisha timu mbalimbali za soka. Timu ambazo zimesajili katika App ya Spocha, zitaweza kupanga ratiba za mechi zao na kujaza matokeo,huku timu hizo pia zikiwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za mechi walizocheza.
Timu ambayo itakuwa imejisajili katika Spocha, itakutanishwa na timu zilizojiunga katika mkoa husika na kutokana na aina ya timu, mathalani timu za Maveterani zitaweza kuwasiliana vizuri na kupanga mechi zao.
Kitu kingine kizuri kupitia Spocha ni kuwa matokeo yote yaliyojazwa katika App hii yataonyesha kila kinara wa mkoa au aina ya kundi ambalo timu ipo,mathalani Makampuni ya Simu, Benki au sekta ya Usafirishaji.
Spocha imebuniwa na kutengenezwa na kampuni ya GALACHA na inapatikana kwa watumiaji wa simu zinazotumia Android tu kwa sasa, katika Google Play. Baada ya majaribio kukamilika Spocha itazinduliwa rasmi.
Timu zote zilizoshiriki mechi hii, Yanga FB Fans na ya wadau wa Kandanda Fc zinapatikana katika Spocha kuanzia sasa, na kama kuna timu inahitaji mechi itatakiwa kupakua na kujisajili katika Spocha na zitatakiwa maombi ya mechi kupitia Spocha tu.
Hivyo makala Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha
yaani makala yote Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/yanga-fb-fans-fc-yapiga-mtu-mkono-wa.html
0 Response to "Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha"
Post a Comment