title : WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU
kiungo : WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU
WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bw. David Beasley hapa nchini ni fursa itakayowawezesha Watanzania kunufaika kwa kiwango kikubwa katika kilimo, uhifadhi na uuzaji wa mazao ya chakula yanayolimwa hapa nchini.
Akizungumza baada ya kukutana na Bw. Beasley jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Julai 27, 2018), Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kuwa na ziada ya chakula msimu wa mavuno utakapokamilika mwaka huu hivyo itahitaji sana kupata soko nje ya nchi ili iweze kuuza ziada hiyo.
Taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa mavuno ya mazao ya chakula kama mahindi, maharage na mbaazi yatafikia tani milioni 16 wakati mahitaji ya chakula kwa Watanzania kwa mwaka ni tani milioni 13, hivyo tutakuwa na ziada ya tani milioni tatu,” amesema.
Akitoa ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Julai 2018 ambapo msimu wa mavuno bado unaoendelea, tayari nchi ina ziada ya tani milioni moja kwani taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonyesha kuwa tayari zimekwishavunwa tani milioni 14.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimikana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley kabla ya mazungumzo yao kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hivyo makala WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU
yaani makala yote WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wfp-itawanufaisha-watanzania-waziri-mkuu.html
0 Response to "WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU"
Post a Comment