title : Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.
kiungo : Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.











Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
SERIKALI imeanza majaribio ya kutoa Dawa za miezi Mitatu hadi sita kwa watu wenye Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kwamba mwakani imepanga kutoa Dawa zenye ubora na ufanisi zaidi mara baada ya Dawa zinazotumika sasa kumalizika.
Mwanzo wa mwaka 2005 hadi sasa , idadi ya watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na wale wanaokufa kutokana na ugonjwa huo nchini inatajwa kupungua, huku takwimu zikionesha mafanikio yanayotokana na juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Tume ya kupambana na UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Wizara ya afya, asasi zisizo za kiserikali na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo endapo juhudi hizi hazitaongezeka, hatari ya ugonjwa huo kuleta madhara bado itakua kubwa na hili ndilo linawaasukuma Mashujaa zaidi ya 70 kushiriki kampeni Dhidi ya Ukimwi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kili Challenge.
Mashujaa hao walioianza safari ya kupanda Mlima huo kupitia njia ya Machame wakiwemo waendesha Baiskeli wamerejea na kupokelewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu na kutangaza Habari njema.
Waziri Mwalimu akaeleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikia malengo makuu matatu ifikapo mwaka 2020 likiwemo la angalau asilimia 90 ya atu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wajue kwamba wana maambuziki .
Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ) Dkt Leonard Maboko ameipongeza kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM) kwa kuratibu zoezi hilo la kuchangisha fedha kwa ajli ya Mapambano Dhidi ya Ukimwi huku akitoa hamasa kwa wadau wengine kujitokeza katika kuchangia fedha kwa ajili ya Mapambano hayo.
Katika safari ya Kupanda Mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia Baiskeli,Washiriki 40 kati ya 45 waliopanda ndio waliofanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru miongoni mwao wakiwa ni Vijana wanne kutoka kituo cha Moyo wa Huruma cha mkoani Geita.
Hivyo makala Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.
yaani makala yote Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-wa-afya-mhe-ummy-mwalimu.html
0 Response to "Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi."
Post a Comment