BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA

BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA
kiungo : BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA

soma pia


BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Hospitali Teule ya mikoa wa Simiyu, Bw. Gigi Mathias akiwaonesha wajumbe wa bodi hiyo mwongozo wa kuendesha bodi hiyo mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Bodi ya Ushauri ya Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu imezinduliwa rasmi na kutakiwa kusimamia vema Hospitali hiyo ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa ipasavyo kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Hospitali hiyo Mjini Bariadi, mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Utawala na Rasilimaliwatu Chele Ndaki, amesema bodi hiyo inalo jukumu kubwa la kuisimiamia hospitali teule ya mkoa na kuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika viwango vinavyotakiwa.

"Mnalo jukumu kubwa katika kuhakikisha kwamba huduma za afya zinazotolewa zinaendana viwango vya Serikali yetu, nafikiri hata ninyi mnaona namna viongozi wetu walivyolipa kipaumbele suala afya, lengo ni kuhakikisha wananchi ambao ndiyo waajiri wetu wapewe huduma nzuri na waendelee kufanya shughuli zao za uzalishaji" alisema Ndaki.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Utawala na Rasilimaliwatu Chele Ndaki, akimkabidhi Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya HospitalI za mikoa, Bw. Gigi Mathias kama ishara ya kuizinda bodi hiyo.

Amesema pamoja na kushauri juu ya namna hospitali inavyotoa huduma, bodi hiyo pia itakuwa na jukumu la kushauri uongozi wa hospitali na kutoa mapendekezo juu ya mambo mbalimbali yanayolenga kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi ili waweze kutoa huduma zinazotakiwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Gigi Mathias amesema wajumbe wa bodi hiyo wamejiwekea mpango kazi utakaowazesha kutoa ushauri ili kuboresha mambo mbalimbali katika hospitali hiyo.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Chele Ndaki akiwaongoza Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Teule ya Mkoa, kutembelea na kuona Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) linalojengwa Eneo la Nyaumata Mjini Bariadi baada ya uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa Hospitali Teule ya Mkoa mjini Bariadi.

"Kama bodi tutaishauri Menejimenti ya Hospitali iweze kuboresha huduma kwa wananchi na watumishi pia kwa sababu kama watumishi hawataboreshewa huduma zao muhimu utendaji wao utakuwa hafifu; tutasimamia rasilimali zote za hospitali, pia tuna jukumu kama bodi kusimamia kandarasi zote na kuhakikisha zinafanya kazi kwa viwango” alisema Gigi.

“Kwa kuwa bodi hii ina wajumbe wengi ambao ni watumishi wa Serikali na wengine ni wastaafu ambao ni wazoefu katika nyanja mbalimbali nina uhakika tutaishauri Menejimenti ya Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu katika masuala yote kwa lengo la kuboresha utendaji na utoaji wa huduma bora" alisisitiza.

Naye Mjumbe wa bodi hiyo Bw. Said Zongo amesema wajumbe wa bodi hiyo watafanya kazi ya kuishauri Menejimenti ya Hospitali Teule ya Mkoa kwa mujibu wa sheria na taratibu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Hivyo makala BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA

yaani makala yote BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/bodi-ya-ushauri-ya-hospitali-teule-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BODI YA USHAURI YA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU YAZINDULIWA"

Post a Comment