title : Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya
kiungo : Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya
Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya
Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kukabidhi magari 47 kwa ajili ya wathibiti wa ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya na magari mawili kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichakoakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa magari hayo kwawathibiti wa ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya na magari mawili kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika gari mara baada ya kuzindua
Sehemu ya magari ya wathibiti wa ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya na magari mawili kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekabidhi magari kwa ajili ya kuimarisha Uthibiti wa ubora elimu.
Jumla ya magari hayo ni 47, ambapo magari 45 ni kwa ajili ya wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya na magari mawili kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo mjini Dodoma Profesa Ndalichako amesema wathibiti ubora wa shule kutumia magari hayo kwa malengo yaliyokusudiwa na hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaotumia magari hayo kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
Amesema kwa mujibu wa Dira yetu ya Maendeleo, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 Tanzania inalenga kujenga uchumi wa Viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Profesa Ndalichako amesema kufikia malengo ya uchumi wa kati Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndiyo yenye dhamana ya kusimamia utoaji elimu, ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha vijana wetu kutoa mchango unaotakiwa katika ujenzi wa uchumi wetu.
Aidha Wizara itasimamia vyema elimu na mafunzo yatolewayo ili kuhakikisha yanakuwa bora na yanatoa mchango wenye tija katika ujenzi wa uchumi wetu.
“Ninathubutu kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inasimamia kwa dhati kabisa jukumu hili la utoaji wa elimu bora kwa kununuaa pikipiki 2,894 ambazo zimesambazwa kwenye Halmashauri 156 katika mikoa 25 kwa ajili ya kusaidia Waratibu Elimu Kata katika kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa shuleni katika maeneo yao.
Hivyo makala Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya
yaani makala yote Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-ndalichako-akabidhi-magari-47.html
0 Response to "Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya"
Post a Comment