title : WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI
kiungo : WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI
WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI
*Lengo ni kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kampeni ya kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma na kuagiza kuanzishwa kwa kituo cha utafiti wa zao hilo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga kilichopo mkoani Kigoma kwa kuwa ndiko zao la Michikichi linalimwa kwa wingi.
Amesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kuhamasisha kilimo cha zao la michikichiki kwa sababu kila mwaka Serikali hutumia zaidi ya sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma, wadau wa zao la michikichi na wabunge wa mkoa wa Kigoma baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku nne inayolenga kuhamasisha maendeleo na kilimo cha zao la Michikichi.Amesema Serikali haiwezi ikaendelea kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje wakati uwezo wa kulima michikichi na kuzalisha mafuta ya mawese kwa wingi tunao, hivyo amewataka viongozi wa Serikali wabadilike na wawafuate wakulima kwenye maeneo ya vijijini na wakawasimamie na kuwashauri namna bora ya kulima zao hilo.
Aidha, ameagiza Wizara ya Kilimo ianze taratibu za kisheria za kukihamisha chuo cha Kihinga kutoka Wizara ya Elimu Sayansi ya Teknolojia kwenda wizara ya Kilimo ili shughuli za tafiti za zao la michikichi lifanyike kwa ufanisi. Pia, ameiagiza Wizara ya Kilimo kuwahamishia mkoani Kigoma watumishi wa kituo cha utafiti wa michikichi cha Bagamoyo ifikapo mwezi Agosti, 2018 isipokuwa wale wanaohusika na utafiti wa zao la minazi tu.
Kadhalika, amewataka viongozi wa mikoa yote inayolima michikichi waanzishe mashamba ya michikichiki ili waoneshe mfano kwa wananchi. “Serikali inataka kuona mabadiliko kwenye zao hili. Sioni umuhimu wa Taifa kuendelea kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha ndani upo,”.
Hivyo makala WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI
yaani makala yote WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-azindua-kampeni-ya-kufufua.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AZINDUA KAMPENI YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI"
Post a Comment