title : Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji
kiungo : Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji
Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kupata mafanikio makubwa kutokana na kuboresha huduma za upasuaji wa watoto, huku ndani ya siku mbili watoto 24 wakiwa wamefanyiwa upasuaji.
Wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Muhimbili wamesema idadi ya watoto wanaofikishwa katika hospitali hiyo kutokana na matatizo mbalimbali, inaeendelea kuongezeka kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo mbalimbali wakiwamo waliozaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa na wengine wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na hewa.Upasuaji wa watoto hao 24 umefanywa na wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri.
Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali hiyo, Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga amesema wataalamu wa muhimbili na wa Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri wameshirikiana kufanya upasuaji mgumu (difficult cases) kwa watoto hao.
Dkt. Mbaga amesema upasuaji huo umekuwa ukifanywa mara kwa mara na wataalamu wa Muhimbili kwa muda mrefu na kwamba katika siku mbili wamekuwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Alexandria kwa ajili ya kubadilisha uzoefu.“Kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa wiki hii tumekuwa na jopo la watalaamu wenzetu 10 wa upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Alexandra kilichopo Misri wakiongozwa na Prof. Saber Mohamed Waheeb mshauri mwelekezi katika upasuaji wa watoto na Dkt. Mohamed Abdelmalak Morsi bingwa wa upasuaji wa watoto,” amesema Dkt. Mbaga.
Madaktari na wataalamu wengine wakiendelea na upasuaji kwa mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa chakula (Gastroeso Phageal Reflux disease).
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Muhimbili na wale wa Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri kufanya upasuaji kwa watoto 24 wenye matatizo mbalimbali. Watoto hao wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi, Dkt. Petronilla Joseph Ngiloi wa MNH, Prof. Saber Mohamed Waheeb kutoka Misri, Dkt. Mohamed Abdelmalak kutoka Misri na Dkt. Ibrahimu Mkoma wa MNH.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri wakifanya upasuaji kwa mmoja wa watoto ambaye ana tatizo kwenye mfumo wa chakula (Gastroeso Phageal Reflux) disease) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Prof. Saber Mohamed Waheeb kutoka Misri, Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga wa Muhimbili na Dkt. Mohamed Abdelmalak kutoka Misri wakifanya upasuaji.
Dkt. Julieth Magandi wa Muhimbili akipokea zawadi kutoka kwa Prof. Saber Mohamed Waheeb wakati wa mkutano wa wataalamu hao na waandishi wa habari leo.
Hivyo makala Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji
yaani makala yote Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/muhimbili-yaendelea-kupata-mafanikio.html
0 Response to "Muhimbili Yaendelea Kupata Mafanikio, Watoto 24 Wafanyiwa Upasuaji"
Post a Comment