WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA
kiungo : WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

soma pia


WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga Kata ya Kisanga wilaya ya Sikonge tarehe 12 Julai, 2018. Wengine wanaoshuhudia ni Viongozi Waandamizi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Sikonge, REA, TANESCO, Wakandarasi pamoja na wananchi.

NA RHODA JAMES - SIKONGE
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jana tarehe 12 Julai, 2018   amewasha rasmi umeme  katika kijiji cha Kisanga kata ya Kisanga wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora.
Waziri Kalemani amewasha umeme huo baada ya kufanya uzinduzi wa mradi husika mwaka jana wilayani Sikonge.
“Leo nimekuja kuwasha umeme, kukagua utekelezaji wa mradi wa REA hapa Sikonge na kuwakabizi Wakandarasi ili kumalizia vijiji vilivyobakia,” alisema Waziri Kalemani.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Sikonge ina jumla ya vijiji 71 na hadi sasa vijiji 30 tayari vina umeme ingawa sio kikamilifu, vijiji 40 vilivyobakia vyote vitapelekewa umeme.
Aliongeza kuwa, mradi huu wa REA III awamu ya kwanza takriban vijiji 26 vitaletewa umeme, vijiji 4 vipo off gridi kwa hiyo vitapatiwa umeme wa Jua (Solar) na vijiji vingine 11 vilivyobakia vitaendelea kuunganishiwa umeme.
“Wakandarasi hawa watawaletea umeme Kijiji kwa Kijiji, Kitongo kwa Kitongoji, Nyumba kwa Nyumba bila kuruka nyumba yoyote” alisisitiza Waziri Kalemani.
Pia, Waziri Kalemani aliendelea kuwahimiza Wafanyakazi wa Halmashauri kutenga pesa kwa ajili ya kuunganishia umeme Taasisi zote za Umma.
Alisema kuwa, ikiwa suala la kutenga pesa hiyo itakuwa ngumu basi, Ofisi zenye chumba kimoja hadi vitatu wekeni kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji wiring ili taasisi zote za umma zipate nishati hii ya umeme.
Aidha kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakuda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge alimshukuru sana Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kwa ushirikiano mkubwa anaoendelea kumpa na kusema kuwa wananchi wa Sikonge wanahitaji umeme ili kuendelea kufungua Viwanda vidogo vidogo na hata kuboresha kipato cha kiuchumi katika miongoni mwao.

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akijiandaa kukata utepe na kuwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakuda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge.

  Wananchi wa kijiji cha Kisanga wakisalimia viongozi waliofika katika kijiji hicho.

  Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akiwasalimia wananchi katika mkutano huo wa kuwasha umeme katika kijiji cha Kisanga Kata ya Kisanga.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Gidion Kaunda akiwasalimia wananchi kabla ya zoezi la kuwasha umeme.


Hivyo makala WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

yaani makala yote WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-kalemani-awasha-umeme-kijiji-cha_15.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA"

Post a Comment