Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU

Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU
kiungo : Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU

soma pia


Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU

 Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (kulia) akizungumza wakati akifunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana.
Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (katikati) kuhusu dawa zinazaondaliwa na wataalamu wa Kitengo cha Dawa asili kutoka Chuo cha MUHAS. Wengine ni pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa (wa tatu kulia)

NAIBU Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa wito kwa watafiti wa afya nchini kufanya utafiti ili kubaini sababu na suluhisho kuhusiana na uwepo wa idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupima virusi vya Ukimwi (HIV) hapa nchini.

Dk Ndugulile alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akifunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016/2017 ulioangalia maambukizi mapya na kiwango cha kufubaza VVU, wanawake wanaongoza katika maambukizi mapya lakini ni wepesi kupima na kutumia dawa kikamilifu ikilinganishwa na wanaume.

“Lengo hasa tunahitaji kuona idadi kubwa ya wanaume ikijitokeza kupima VVU ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi mapya ifikapo 2030. Ili tuweze kufanikisha hili ni lazima tuwe na majibu ya kitafiti yatakayotupa muongozo kuhusu sababu za wanaume kukwepa kupima VVU na nini hasa kifanyike kuondoa changamoto hizo,’’ alisema.

Alisema kwasasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa sera ya afya hivyo tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya afya ni muhimu ili kuiwezesha sera hiyo kuhakisi ualisia wa masuala muhimu katika sekta hiyo.

Aliongeza kuwa kwasasa taifa linakabiliwa zaidi na magonjwa yasiyoyakuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, kiarusi pamoja na ugonjwa wa figo huku akitaja sababu kuwa ni pamoja na mfumo wa maisha usiozingatia miongozo ya lishe, matumizi ya pombe kupitiliza na uhaba wa mazoezi miongoni mwa wana jamiii.

“Upande wetu serikali tunaendelea kuboresha huduma za kibingwa kuhakikisha magonjwa kama figo na mengine ambayo tulikuwa tunatumia fedha nyingi kusafirisha wagonjwa nje ya nchi sasa yanatibiwa hapa nchini.,’’ alisema huku akitolea mfano matibabu ya figo ambayo kwasasa yanafanyika ndani ya nchi kwa sh mil 21 badala ya mil 100 zilizokuwa zikitumika nje ya nchi kwa kila mgonjwa.

Kuhusu suala la upatikanaji wa dawa hapa nchini, Dk Ndugulile alisema; “ Kwasasa serikali imetoa muongozo wa utoaji wa dawa ambapo badala ya kuruhusu soko liamue dawa gani zitumike kwasasa serikali ndio inaamua dawa ipi itumike kutibu ugonjwa upi, sehemu gani na kwa utaalamu gani,’’ alisisitiza.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe alisema nyingi kati ya tafiti zilizowasilishwa kwenye mkutano huo wa siku mbili zilijikita katika vipaumbele vya taifa yakiwemo masuala ya HIV/AIDS, kifua kikuu, afya ya uzazi na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ajali pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika.

“Mkutano huu umewakutanisha wataalamu wa afya katika ngazi tofauti wakiwemo wale waliobobea pamoja na wanafunzi ili kuruhusumbadilishano wa mawazo na ujuzi. Zaidi ya tafiti tofauti 200 zimewasilishwa kupitia mkutano huu’’ alisema.

Aliishukuru serikali ya Sweden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huo.


Hivyo makala Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU

yaani makala yote Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/watafiti-wa-afya-waombwa-kubaini-sababu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU"

Post a Comment