title : UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR
kiungo : UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR
UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR
MKURUGENZI wa Kampuni ya Showtime Intertiment Ibrahim Mitawi amesema kuwa wanatarajia kuzindua Kampuni yao ifikapo tarehe 27 mwezi wa saba mwaka huu katika Ukumbi wa Ngome Kogwe Zanzibar.
Hayo aliyasema huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Kampuni ya Showtime Intertiment inayotarajiwa kuanza saa moja Usiku.
Alisema kuwa lengo kuu la uzinduzi wa Kampuni hiyo ni kutaka kuijuilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi kwamba Vijana wa Kampuni ya showtime wanauwezo mkubwa wa kuitangza Zanzibar kiusanii .
Aidha alisema kuwa Zanzibar ni Kisiwa cha Utalii hivyo watahakikisha kupitia Kampuni yao kwa kutumia vipaji walivyonavyo kuhakikisha wanaitangaza Zanzibar kupitia Matamasha mbali mbali ili kuimarisha Utalii utaoengeza uchumi wa Nchi.
Hata hivyo alisema kuwa hawatoweza kuacha Utamaduni wao hivyo katika ufunguzi wa Kampuni hiyo kutakuwepo burudani mbali mbali za Utamaduni wa asili.
Hata hivyo Ibrahim Mitawi alisema ili Sanaa ifike mbali zaidi kuutangaza Utalii ni muhimu kuwepo na mashirikiano baina ya Makampuni mbali mbali pamoja na Serikali.
Msemaji wa Showtime Intertinment Musilim Nassor akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Uzinduzi wa Showtime itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi akitoa ufafanizi wa masuali aliyokua akiulizwa na Waandishi juu ya Uzinduzi wa Showtime hiyo itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar (kushoto) ni Saleh Nassor Abdallah ( Dj CARTEL) na Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa.
Mwandishi wa Habari wa Gaziti la Majira Mwajuma Juma akiuliza maswali katika mkutano kuhusiana na Show hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 27/07/2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa akijibu baadhi ya maswali yaliokua yakiulizwa na Waandishi kuhusiana na Show hiyo (kulia) ni Dj CARTEL, Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi na Msemaji wa Taasisi hiyo Musilim Nassor. Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR
yaani makala yote UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/uzinduzi-wa-showtime-entertainment.html
0 Response to "UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR"
Post a Comment