title : MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI
kiungo : MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI
MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Matayarisho ya matengenezo ya Jengo la Kihistoria la Mji mkongwe la Beit el Ajaib yameanza rasmi kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Makarani Sariboko alieleza hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi yanavyoendelea katika jengo hilo Forodhani.
Alisema ujenzi wa jengo hilo mashuhuri katika Ukanda wa Afrika Mashariki lililoporomoka mwaka 2012 litagharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni nne na nusu na matengenezo yake yatachukua miezi 18.
Aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wataalamu wazalendo wamemaliza kufanya uchambuzi wa matengenezo hayo na kazi ya ujenzi wa jukwaa kuelekea sehemu ya juu unaendelea.
“Tayari wataalamu wetu wamemaliza kufanya ufafanuzi wa jumba lote kuanzia sehemu ya juu iliyoporomoka, sehemu za ndani na eneo la chini ya ardhi ya jengo hilo’’, alisema Mkurugenzi Makarani.
Alisema kutakuwa na mchanganyiko wa timu ya wataalamu kutoka nchi za nje na wataalamu wazalendo wa Zanzibar ili kupata ufanisi mzuri wa ujenzi huo.
Nae Mkurugenzi wa Makumbusho Salim Kitwana Sururu alisema Serikali ya Oman ilifikia makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kulifanyia matengenezo jengo hilo la kihistoria lililohifadhi kumbukumbu muhimu za tawala zilizopita.
Muhandisi wa Mji Mkongwe Suhad Sultani Alawi alitoa wito kwa wananchi wanaotumia eneo hilo kuwa tahadhari kubwa wakati wa matengenezo ya jengo hilo kwa kulinda usalama wao.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Hivyo makala MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI
yaani makala yote MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/matayarisho-jengo-la-kihistoria-mji.html
0 Response to "MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI"
Post a Comment