TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI

TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI
kiungo : TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI

soma pia


TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuongeza tija kwa wataalam wa ndani mara baada mradi wa ujenzi wa rada nne kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, amesema kuwawezesha wataalam wa ndani kutawajengea uwezo wa kwenda na kasi ya teknolojia kwenye uongozaji ndege.

“Mradi huu utatumia fedha nyingi hivyo ni vyema kuzingatia wataalam wa ndani kupata elimu ya rada hizi ili mradi ukikamilika wasimamie vyema na si watalaam kutoka nje ya nchi”, amesisitiza Mhe. Kakoso.Mhe. Kakoso, amesema kuwa Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa rada unaoendelea na kuwataka mradi ukamilike kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, amesema uboreshaji wa Viwanja vya ndege mbalimbali nchini unafanywa kwa pamoja na ufufuaji wa Shirika la Ndege ambapo mpaka sasa Serikali imeshanunua ndege sita.Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari ameihakikishia Kamati kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango na kusema kuwa tayari kuna wataalam zaidi ya 20 ambao watapata mafunzo ili kuongoza rada hizo mara baada ya mradi kukamilika.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga, Aristide Kanje akiwaonesha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu eneo la Chuo hicho, wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara chuoni hapo, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso
Muonekano wa jengo la rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambalo linaendelea kujengwa, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa rada ya kisasa inayosimikwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari (Kushoto), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya mafunzo, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa gari jipya la Zimamoto lililonunuliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA). Gari hilo litatoa huduma katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.




Hivyo makala TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI

yaani makala yote TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tcaa-yashauriwa-kuwekeza-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI"

Post a Comment