title : Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake
kiungo : Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake
Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA Jennifer Mushi anayekabiliwa na kesi ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh. Mil 197 wakati wa uhakiki wa mali zake, walibaini kuwa na magari 10 ambayo hayakutamkwa.
Afisa Mchunguzi wa TRA, Tumaini Fadhir ameieleza hayo leo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Akiongozwa na wakili wa serikali, Vital Peter amedai baada ya kupitia fumo za matamko mbali mbali ya Mali na madeni, walibaini magari zaidi ya kumi yaliyoonekana kwenye miliki za mshtakiwa yakiwa hayajatamkwa kwa mujibu wa taratibu.
"Nilifanya uchunguzi wa mali zote zinazohusika na zisizohusika na kibaini kuwa magali hayo hayakutamkwa ukichilia, magari hakuna mali zingine tulizobaini", amedai Tumaini.
Amedai kuwa, baada ya kubaini hayo, alitoa taarifa kwa menejimenti.
Katika ushahidi wake, Tumaini amedai yeye ni mchunguzi wa ndani wa TRA, huku majukumu yake ni kuchunguza malalamiko ya watumishi, kuhakiki mali za watumishi zinazohusu matamko ya mali na madeni kwa lengo la kuthibiti vitendo vya rushwa.
Aidha akihojiwa na wakili wa uetezi Furgence Masawe kama anamfahamu Jennifer, alijibu kuwa anamfahamu kwa sababu aliwahi kumchunguza.
Pia aliulizwa kama anafamu idadi ya mali za Jennifer na thamani yake , Tumaini alijibu anafahamu.
Pia aliulizwa Jennifer alianza kazi lini TRA, alijibu kuwa tangu mwaka 2011 lakini awali aliajiriwa katika sekta binafsi.
Baada ya kutolewa ushahihidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi August 16,2018.
Jenifer anakabiliwa na kosa la kumiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake, anadaiwa aliyaingiza magari hayo nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 197,601, 207.
Hivyo makala Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake
yaani makala yote Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/shahidi-katika-kesi-ya-kumiliki-mali.html
0 Response to "Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake"
Post a Comment