title : WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI
kiungo : WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI
WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI
Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini wamesisitizwa kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kusaidiwa. Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa wito huo hivi karibuni Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, kwenye mkutano wake na Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Dhahabu na Vito (Green Garnet) wa Namungo wilayani humo.
Nyongo alisema dhamira ya Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwa na uchimbaji wenye manufaa kwao na Taifa kwa ujumla na ili kufikia dhamira hiyo ni vyema wakajiunga kwenye vikundi. "Mkijiunga kwenye vikundi itakua ni rahisi kuwafikia kwa pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali yenye tija kwenye shughuli zenu," alisema.
Alisisitiza kwamba umoja ni nguvu, na ili mchimbaji awe na uwezo na nguvu kwenye utekelezaji wa majukumu yake inabidi afanye kazi akiwa ndani ya umoja na wenzake. Alisema pale ambapo wachimbaji watakua wamejiunga kwenye vikundi, itakua rahisi hata kwa Taasisi za kifedha kuweza kuwafikia na kuwasaidia ikiwemo kuwapatia elimu ya fedha na vilevile mikopo.
"Nimekuja hapa kuzungumza nanyi ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi, na pia ninawaasa mhakikishe mnajiunga kwenye vikundi," alisema. Aliongeza kwamba Serikali ingependa kuona Wachimbaji Wadogo wa Madini wanafanikiwa kufikia kwenye uchimbaji wa Kati na baadaye kuwa Wachimbaji Wakubwa.
Aidha, Wachimbaji hao walimuomba Naibu Waziri Nyongo kuendelea kuwatembelea mara kwa mara ili kuelewa changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi kila inapobidi. Baada ya kuzungumza na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo alitembelea Mgodi wa Dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Germin Exploration ya Namungo huko Ruangwa na kukagua shughuli zinazofanywa na mgodi huo.
Vilevile alitembelea mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika vijiji vya Mtondo na Nanjaru wilayani humo ambapo aliahidi kuwasaidia kumaliza tatizo la upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi wanayohitaji ili mradi uweze kuanza mara moja.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza alipotembelea Mgodi unaomilikiwa na Kampuni ya Germin Exploration.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akipata maelezo ya Mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika kijiji cha Mtondo na Nanjaru wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alipotembelea na kuzungumza na Wachimbaji kwenye Miradi ya kuchimba Madini ya Dhahabu na Kinywe Wilayani Ruangwa.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akipata maelezo ya Mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika kijiji cha Mtondo na Nanjaru wilayani humo.
Hivyo makala WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI
yaani makala yote WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/wachimbaji-wadogo-wa-madini-watakiwa.html
0 Response to "WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI"
Post a Comment