title : BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu
kiungo : BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu
BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza leo kuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe amejiuzulu.Spika Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii. Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.
Hivyo makala BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu
yaani makala yote BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/breaking-newzzzz-rais-robert-mugabe-wa.html
0 Response to "BREAKING NEWZZZZ: Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu"
Post a Comment