title : POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO
kiungo : POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO
POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Polisi Jamii wawili na dereva mmoja wakazi wa Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 239.5.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Faraja Nguka aliwataja washtakiwa hao kuwa ni dereva mkazi wa Mbezi Luis, Kefas Mlenzi (30), Polisi Jamii, Juma Mtali (35) na Polisi Jamii, Greyson Muhapa maarufu kama Masu (32) wote wakati wa Mbezi Luis.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Ally Salum, wakili Nguka amedai Juni 28/ 2018 huko Mbezi katika Wilaya ya Ubungo washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa na vipande 30 vya meno ya tembo vyenye thamani USD 105,000 sawa na Sh 239,505,000 bila ya kuwa na Kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.
Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za uhujumu uchumi, isipokuwa mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP
Kesi imeahirishwa hadi Julai 23, 2018 kwa mijibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hivyo makala POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO
yaani makala yote POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/polisi-jamii-wawili-kizimbani-kwa.html
0 Response to "POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO"
Post a Comment