title : Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi.
kiungo : Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi.
Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake.
Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi naye akikumbana na kadhia hiyo.
Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu.
Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
“Ndugu zangu wakati Rais akiniteua aliniagiza nihakikisha wananchi wanapata 1maji vinginevyo nitatumbuliwaa nami sipo tayari kwa hilo hivyo nitahakikisha tunawachukulia hatua kali wakandarasi wanaoshindwa kuendena na kasi na hivyo kuikwamisha kwa maslahi yao binafasi huku wananchi wakiendelea kuteseka”Alisema.
Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita alimuelezwa Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo umejengwa chini ya kiwango na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka na adha ya maji.
“Mh Naibu Waziri wilaya ya Handeni ni miongoni mwa wilaya ambazo zinachangamoto kubwa ya tatizo la maji lakini sisi kama wabunge tumekuwa tukiiomba fedha za mradi ya maji lakini wakandarasi wamekuwa wakitukwamisha”alisema.
Alisema kinachofanywa na wakandasi hao juu ya utekelezaji wa miradi hii ni ubadhirifu wa wazi kabisa hivyo ili kuondokana na tatizo hilo serikali inapaswa kuwachukulia hatua wakandarasi wa namna hiyo ili iwe fundisho wa wengine wenye tabia za namna hiyo.
Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema miradi hiyo ambayo Rais aliagiza imalizike leo (jana)Julai 23 huku jambo la kushangaza hakuna dalili ya umalizikaji wa miradi hiyo. Miradi hiyo ambayo ilitakiwa kutelezwa Wilayani hapo ni pamoja na bwawa la mkata,bwawa la manga na miundombinu ya mambomba toka katika bwawa la mkata hadi mkata mjini jambo ambalo halijafanyika hadi mwisho wa agizo
Hivyo makala Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi.
yaani makala yote Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-mheaweso-aamuru-kuwekwa.html
0 Response to "Naibu Waziri Mhe.Aweso Aamuru Kuwekwa Ndani Wakandarasi wa Mradi wa Handeni Kwa Kushindwa Kuwepo Eneo la Mradi."
Post a Comment