title : NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA
kiungo : NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA
NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akipita katika kichaka kuelekea katika kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa nchi hizo mbili eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akitafuta kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kwa kuchimba eneo ambalo kigingi hicho kilikuwepo katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga. Nyuma zinazoonekana nyumba zimejengwa katikati ya mpaka huo wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia baadhi ya nyumba zilizojengwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya katika kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkinga mbele ya nyumba iliyojengwa upande ukiwa Tanzania na mwingine Kenya, kuanzia diwani Hassan Bakari Ally (wa nne kulia aliyevaa kofia) kuelekea kulia wako upande wa Kenya.wengine ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki (wa pili kulia) na wa tatu kushoto ni mbunge wa jimbo la Mkinga Dustan Kitandula.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akioneshwa kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kilichowekwa wakati wa utawala wa muingereza na Mwenyekiti wa kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga Nassoro Mbarouk Nassoro wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akieleza jambo mara baada ya kupata maelezo juu ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha Saruji,nishati ya umeme joto, mabegi, vifaa vya ujenzi pamoja na bandari ndogo katika eneo la Mtimbwani wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki wakati alipofanya ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akipata maelezo kuhusiana na mpaka wa Tanzania na Kenya kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mahandakini Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga Nassoro Mbarouk Nassoro wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki na wa nne kulia ni Mbunge wa jimbo la Mkinga Danstan Kitandula.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi)
………………………………………………………………………..
Na Munir Shemweta, Mkinga Tanga
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.
Katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha umbali wa mita mia kama eneo huru.
Eneo lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake wamejenga nyumba zao zikiwa karibu kabisa na mpaka huku baadhi yake sehemu ikiwa upande wa Tanzania na nyingine upande wa Kenya.
Hata hivyo, Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshuhudia upande wa Tanzania katika eneo la Horohoro ukiwa umezingatia umbali unaotakiwa kati ya mpaka ukilinganisha na wakenya wanaoishi kijiji cha Jua kali Lungalunga ambao wamejenga karibu kabisa na mpaka wa Tanzania.
Kufuatia hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wakazi wanaoishi katika maeneo hayo ya mpakani kukumbwa na zoezi la kubomolewa nyumba zao ingawa kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea baina ya Tanzania na Kenya kuhusu umbali gani pande hizo zinaweza kukubaliana ili kunusuru baadhi ya wananchi wa pande zote mbili.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema, kwa sasa umbali unaotambulika kama eneo huru baina ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja ingawa kuna mazungumzo yanayoendelea katika ngazi ya wataalamu juu suala la umbali wa eneo huru.
Kwa mujibu wa Mabula, pamoja na sheria kuweka bayana kuwa umbali unaotakiwa katika eneo huru kati ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja lakini pande hizo zinaweza kukubaliana kama ilivyofanyika kwa nchi ya Uganda na Burundi ambapo kwa Uganda eneo huru litakuwa mita thelathini huku Burundi likiwa mita kumi na mbili na nusu.
Amesema, ukaguzi wa mipaka anaoufanya una lengo la kuhakikisha mipaka ya Tanzania na nchi jirani inakuwa katika hali nzuri hasa ikizingatiwa alama za mipaka zilizopo ni za muda mrefu huku baadhi yake zikiwa zimeharibika.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesisitiza kuwa, kwa sasa Tanzania haina mgogoro na Kenya juu ya mipaka na kinachofanyika ni kuimarisha usalama wa nchi zote mbili hasa ikizingatiwa njia za panya ziko nyingi.
Mabula amesema, awamu ya kwanza ya kuweka alama za mipakani itafanyika katika mipaka baina ya Tanzania na Kenya pamoja na mpaka kati ya Tanzania na Uganda na fedha yote kwa ajili ya kazi hiyo imeshatolewa kinachosiriwa ni kuanza tu kwa zoezi..
Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula kuwa Wilaya yake imekuwa lango la raia wanaokimblia afrika kusini, dawa za kulevya kama mirungi na mpango wa wilaya ni kutaka kufyeka miti na vichaka vilivyopo katika mpaka kati ya Tanzania na Kenya.
Aidha, amesema wilaya ya Mkinga ina tatizo la wahamiaji waloweza na zoezi la kuwatambua limeanza ili kuwabaini sambamba na kuthibiti vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amehitimisha ziara yake ya siku kumi na mbili mkoa wa Tanga, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na uhamasishaji ulipaji kodi hiyo ambapo ziara ilianzia mkoa Mara, Arusha na Kilimanjaro.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/naibu-waziri-mabula-abaini-ujenzi-wa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI MABULA ABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA"
Post a Comment