title : MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER
kiungo : MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER
MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa yupo tayari kuwajibu watu wote ambao wataonekana kubeza ujio wa ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati anatoa utambulisho kwa Rais Dk.John Magufuli kuhusu baadhi ya wageni waliofika kushuhudia tukio la ujio wa ndege hiyo.
Hivyo ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Rais Magufuli kutowajibu wote ambao watabeza ujio wa ndege hiyo katika mitandao ya kijamii na kwamba kazi ya kuwajibu ataifanya yeye na kuungwa mkono na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Naomba nitoe ombi kwako Rais umekuwa ukitufanyia mambo makubwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.Hata hivyo nikuombe usiwajibu watu ambao watabeza ,kazi hiyo nitaifanya mimi tena kwa kuwafuata huko huko mitandaoni.“Rais ukiwa pale Ikulu endelea tu na mipango yako ya kuwafanyia maendeleo Watanzania wote, hili la kuwajibu wanaobeza mambo makubwa ambayo unayafanya tutafanya sisi,”amesema Makonda.
Amemsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo ambayo Watanzania wanayoana na wale ambao hawataki kuyaona basi watege masikio yao vizuri.“Ndege hii najua leo itakuwa kwangu na baadae itakwenda Mwanza, Arusha na Mbeya.Hata hivyo ndege hii itakwenda zaidi ya Bara la Afrika.
“Yoyote ambaye anapinga kinachofanyika maana yake anapingana na ukweli.Kuna mafanikio makubwa yanaonekana na ambaye haoni basi atege masikio yake vizuri asikie,”amesema Makonda.
Hivyo makala MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER
yaani makala yote MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/makonda-asema-atawajibu-wote.html
0 Response to "MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER"
Post a Comment