title : KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE
kiungo : KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE
KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE
Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.
Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.
Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, wakionekana wenye furaha wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene akipeana mkono na Katibu Mkuu Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
RUBANZIBWA-- Mh. George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE
yaani makala yote KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/kila-shule-itakayohitaji-usajili-lazima.html
0 Response to "KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE"
Post a Comment