title : MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU.
kiungo : MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU.
MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU.
Na Agnes Francis,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Golden boy promotion wakishirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa ngumi za kulipwa, wamewakutanisha mabondia wa hapa nchini kujadili maendeleo ya tasnia hiyo.
Ambapo wanafanya maandalizi ya kukutana na Serikali ili kuwatambulisha mabondia hao na Taifa liweze kuwatambua kuwa ni kitu gani huwa wanakwenda kufanya katika mapambano yao pamoja na kuwapa zawadi kama motisha kwao.
Promota wa ngumi za kulipwa hapa nchini Shomary Kimbau akizungunza na vyombo vya habari katika hotel ya The Cage sports kurasini Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa sasa ni wakati wa mambondia hao kujulikana na Watanzania kwa kazi wanayoifanya ndani na hata nje ya nchi.
Kimbau amesema kwa mwaka huu kuna vijana watano wameshinda mikanda nje na kurudi nayo nyumbani ,lakini hawakuweza kutambulika katika jamii kwa kulitangaza Taifa letu na kufanya vizuri."Kuna bondia mmoja anaitwa Maono Ally ameshinda mkanda mkubwa wa WBC huko nchini Afrika kusini kwa nokauti raundi ya 2,tangu karudi hakuna mtu aliempa zawadi au kwa kumpongeza kwa sababu pia hajulikani"amesema kimbau
Promota huyo amesema kwa kutambua hilo wataungana na wadau mbali mbali hapa nchini septemba Mosi mwaka huu kuwapa zawadi mabondia wote waliowahi shinda mikanda ndani na nje ya nchi.Ambapo siku hiyo wanatarajia mgeni rasmi kuwa Waziri wa habari utamaduni na michezo Harrison Mwakyembe,hafla hiyo itaambatana na burudani ya mipambano minne ya ndondi.
Bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla amewashukuru wadau hao kwa kuanzisha programu hiyo ambayo ni ya mara ya kwanza,vile vile ametoa wito kwa serikali indelee kuunga mkono na wadhamini wajitokeze kama ilivyo michezo mingine.
Bingwa wa ngumi za kulipwa hapa nchini Ibrahim Clasic amesisitizia kuwa programu hiyo ilioanzishwa iwe endelevu kwa kuwa italeta mapinduzi ya mchezo huo na vijana watajitokeza kwa wingi.
Promota wa ngumi za kulipwa Tanzania Shomary Kimbau akizungumza katika hotel ya The Cage sports mivinjeni Jijini Dae es Salaam leo,kuhusu programu ya kuwatambulisha mabondia walioshinda mikanda mbali mbali ndani na nje ya nchi pamoja na kupewa zawadi Septemba Mosi mwaka huu,Bondia wa zamani Rashid Matumla katikati,Bingwa wa ngumi za kulipwa Tanzania Ibrahim Classic kulia.
Hivyo makala MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU.
yaani makala yote MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mabondia-nchini-kupewa-zawadi-septemba.html
0 Response to "MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU."
Post a Comment